Header Ads

Responsive Ads Here

MKANDARASI APEWA MIEZI KUMI KUKAMILISHA BARABARA YA TABORA HADI PANGALE.


kiwango
Na Tiganya Vincent-RS-TABORA
 
Serikali imemwagiza Mkandarasi anayojenga barabara kutoka Tabora hadi Pangale kuhakikisha anakamilika ifikapo mwakani Mwezi Mei la sivyo atafukuza na atapata kazi tena hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbawara wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara mkoani hapa.
Alisema kuwa barabara hiyo imechukuwa muda mrefu na ujenzi wake umekuwa ukienda kwa kasi ndogo na kusababu usumbufu kwa abiria na wasafirishaji wa mizigo katika barabara hiyo.
Profesa Mbawara alisema kuwa Mwezi Mei mwakani ndio muda wake wa mwisho na kama atakuwa hajakamilisha Serikali italamizika kumfuka na asitarajie kupata ya aina yoyote hapa nchini labda nje ya Tanzania.
Waziri Mbawara aliwaomba watumiaji wa barabara hiyo kuwa wavumilivu kwani Serikali inamfuatilia Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha barabara hiyo ifikapo mwakani na ikiwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi alisema barabara hiyo itakapokamilika itayafungua maeneo mbalimbali ya Mkoa huo ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abira na kuinua uchuni wa eneo hilo.
Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo yeye na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wamekuwa wakifuatilia ujenzi wake ili kuhakikisha inakamilika kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa Wanatabora.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuboresha miundo mbinu ya usafiri wa aina mbalimbali Mkoa wa Tabora .
Naye Meneja wa Tanroads Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze alisema wanaendelea kupambana na Mkandarasi kuhakikisha kuwa kazi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Alisema mradi huo ni mdogo ambao una urefu wa kilometa 30 ukilinganisha na miradi mingine lakini Mkandarasi amechelewa kumaliza na kuongeza kuwa Waziri akija tena kama atakuwa hajamaliza ni vema akamfukuza.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 30 unajengwa na Kampuni ya CZCO kutoka nchini China.

No comments