Header Ads

Responsive Ads Here

Mhe. Mrisho Gambo azindua sensa ya watu,mifugo na makazi wilayani Ngorongoro

index
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amezindua sensa ya watu,mifugo na makazi katika kata ya Ngorongoro ambayo kwa sehemu kubwa ipo ndani ya hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro ikiwa ni maagizo ya waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwezi Desemba 2016 katika ziara yake mkoani Arusha.
Akizungumza na wananchi wa tarafa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Takwimu ya Taifa Bi Joy Sawe amesema lengo ni kujua kiasi cha shughuli za kibinaadamu katika eneo hilo ili serikali iweze kupanga mipango yake ya kiuchumi kwa usahihi. Pia amesema wao kama ofisi ya Takwimu ya Taifa wanawashukuru sana wananchi wa Tarafa hiyo kwa ushirikiano wanaowapa kwani hii ni mara yao ya kwanza kuendesha zoezi kama hili, hivyo mafanikio ya zoezi hili yatawapa uzoefu mkubwa kuliendesha katika maeneo mengine.
Naye Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro  Bw. Rashid Mfaume Taka amewataka wananchi wa tarafa hiyo kuendelea kuwapa wataalamu hao ushirikiano kwani zoezi hili lina manufaa makubwa kwao, na pia baada ya zoezi hili wajiandae kwa zoezi la uwekaji alama mifugo ambalo litasimamiwa na wanakijiji wenyewe ili kuwaondoa hofu wananchi hao.
Akizungumza na wananchi hao Mhe. Gambo amewaambia wananchi hao hawana haja ya kua na hofu na serikali yao kwani ina lengo zuri katika kuboresha maisha yao na ustawi wa mamlaka ya Ngorongoro.
“Nyinyi wenyewe ni mashahidi wa namna ambavyo hifadhi hii ya mamlaka ya Ngorongoro inavyojitoa katika kuboresha maisha yenu, lengo la sensa hii ni kujua ni wakazi kiasi gani na mifugo kiasi gani iko eneo hili kwani kuna baadhi watu ambao sio wakazi halali wa eneo hili wamekuja na mifugo hali ambayo ina hatarisha ustawi wa hifadhi yetu” alisema Gambo.
Pia amewaonya wale wote ambao wanaweka siasa katika kila jambo, ” yeyote atakayekwamisha zoezi hili namuhakikishia tutahangaika nae hakuna siasa katika zoezi hili” alionya Mhe. Gambo.
Zoezi hili litafanyika kwa muda wa siku kumi na linafanywa na vijana 138 wa tarafa hii ambao wamepewa mafunzo ya kutumia dodoso la kieletroniki katika ukusanyaji wa taarifa

No comments