Header Ads

Responsive Ads Here

MH. ANTHONY MAVUNDE amezindua mpango wa Urasimishaji wa Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo


vun2
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE amezindua mpango wa Urasimishaji wa Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo kwa vijana wa Kanda ya Magharibi Mkoani Kigoma na kuwataka vijana kujitokeza kuchangamkia fursa za Mafunzo zinazotolewa na Serikali ili waweze kushiriki katika kujenga Uchumi imara kupitia Mapinduzi ya Viwanda.

Mhe MAVUNDE amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kugharamia mafunzo kwa Vijana elfu tatu Mia tisa 3,900 katika maeneo mbalimbali nchini hatua ambayo itawasadia kuwajengea uwezo vijana  kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa kupitia Mapinduzi ya Viwanda ambapo baada ya mafunzo Serikali itawasaidia vijana kuanza kujiajiri kupitia viwanda vikubwa na vidogovidogo katika maeneo yao.
Awali Akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa Mpango huu, Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Mhe Zitto Zuberi Kabwe amempongeza Naibu Waziri Mavunde pamoja na Serikali kwa kuzindua Mpango huu utakaosaidia Vijana wa Vyama vyote vya siasa, pamoja na Dini zote pasipo ubaguzi.
Mhe Zitto amesema katika uchumi wa Sasa wa Dunia nguzo pekee kwa vijana kufanikiwa baada ya Kupewa Mafunzo ni kujiunga katika vikundi vya umoja ili waweze kufikiwa kwa haraka na Serikali katika kupatiwa Mikopo na fedha zinazotengwa kwa ajili ya makundi ya vijana,na wanawake itakayowasaidia kujiajiri wenyewe.
Mpango huu unafadhiliwa kwa asilimia Mia moja na Serikali na unatekelezwa kwa pamoja na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA, ambapo kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA Bi. Leah Lukindo amewahakikishia vijana kuwa watatumia mtandao wa vyuo vya VETA kuwafikia vijana ambao ndio walengwa wa kuu wa mpango huo katika maeneo mbalimbali nchini.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu. 
13/07/2017

No comments