Header Ads

Responsive Ads Here

Mbunge wa Jimbo Muheza, Balozi Adadi Rajabu akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), ameneo mbalimbali yaliyoathiriwa na wachimbaji wa madini katika eneo hilo ambalo ni muhimu kutokana kuwa na chanzo cha maji ambayo yanatumika katika eneo kubwa mkoani Tanga. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanaasha Tumbo.


PIX 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), akiongozwa na Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina kumuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi ambalo linasambaza maji sehemu kubwa ya Jiji la Tanga ambalo limeharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo wakidai kuwa wanatafuta madini ya dhahabu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi linafanya oparesheni katika eneo hilo mara kwa mara na pia linatarajia kujenga Kituo cha Polisi katika eneo hilo ili kupambana na wahalifu hao. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Muheza, Oscar Joshua, na kulia ni Mshauri wa Wagambo wilayani humo.  


PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Mhifadhi Msaidizi Hifadhi ya Asili Amani, wilayani Muheza, Bob Matunda (wapili kushoto), alipokua anamuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi lililoharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimbo wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo. Masauni aliongozana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya muda wa usiku kwenda kuangalia waharibifu hao walivyoliharibu eneo hilo.  
PIX 3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo (kulia), mara baada ya kuangalia eneo la chanzo cha maji katika hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani ambalo liliharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo katika eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji, wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo.  Masauni akiongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, walifika eneo hilo la tukio muda wa usiku.  Katikati ni Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina.

PIX 4
Mbunge wa Jimbo Muheza, Balozi Adadi Rajabu akimuonyesha  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na wachimbaji wa madini katika eneo hilo ambalo ni muhimu kutokana kuwa na chanzo cha maji ambayo yanatumika katika eneo kubwa mkoani Tanga. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanaasha Tumbo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments