Header Ads

Responsive Ads Here

Mavunde akonga nyoyo za wajasiriamali Dodoma


waj
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akizungumza wakati alipofungua kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini leo.

waj1
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali mbalimbali mara baada ya kufungua kongamano hilo.
……………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde amesema suala la kuwainua na kuwapatia elimu ya  ujasiriamali wananchi kwa azma ya kuendesha biashara zao kitaalam na kwa mpangilio utakaokuza vipato vyao kiuchumi ni mkakati endelevu wa kufa na kupona imefahamika.
Mavunde ambaye pi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu leo alifungua kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mjasiriamali Kwanza.
Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Cavillam mjini hapa zaidi ya washirikishi 2000 wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa , kuchota  elimu ya ujasiriamali kwa siku nne na baadaye kuunda na kusajili vikundi vya ujasiriamali ambapo ofisi   ya Mbunge wa Dodoma Mjini imeahidi kuvitafutia fursa  na kuvisimamia.
Alisema kimantiki na kimkakati vikundi hivyo vitapatiwa mbinu za kitaaluma na fursa za kuweza kujipatia  mikopo na mitaji ya kufanya shughuli zao, baada ya kujengewa uwezo na kupatiwa  elimu kuhusu mafunzo ya ujasiriamali na wajasiriamalu hao
“Tutaanza kugawa kwa vikundi zikiwemo  mashine za kutengeneza chaki,mashine ya kutotoleshea mayai (Incubators)za  kutengeneza matofali za kunyonyoa manyoya ya kuku (chicken pluckers) za kushonea, zikiwemo na za kukamua juice” Alisema Mavunde.
Aidha alisema pia zitatolewa mashine za kukamlia miwa na za  kutengeneza popcorn na zile za kuchapisha yaani (heat press) ambapo jumla  gharama za.mashine zote ni shiling milioni 52.
Hata hivyo mbunge huyo alisisitiza kuwa kupitia mpango kazi wa jimbo la Dodoma Mjini,  wajasiriamali hao  watapatiwa fursa za kukuza vipato vyao kiuchumi na kwa mtu mmoja mmoja na hivyo kujijenga vyema kimaisha baada ya kuchangamkia fursa za  uwepo wao katika Makao Makuu ya Serikali Dodoma.
Mavunde ambaye wananchi jimboni mwake akifahamika kwa jina la “De populo Servorum” yaani Mtumishi wa watu,  aliahidi atakuwa  bega kwa bega na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa  kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM  ya Mwaka 2015/2020 pia akishirikiana na mashirika hiari ya kijamii, NGOS na taasisi zinazofundisha masomo ya biashara , utiaji wa elimu na mbinu za kukuza ujasiriamali na watu kujitegemea.

No comments