Header Ads

Responsive Ads Here

MASHINDANO YA ARC KUZINDULIWA AGOSTI 4 MWAKA HUU NA WAZIRI MWAKYEMBE JIJINI DAR ES SALAAM


a02bac9b-db7d-4291-ae50-1a594942a1ed-750x375
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajiwakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya ARC ambapo yatazinduliwa siku ya  Ijumaa ya Agosti 4, 2017, Jijini Dar es Salaam na ambapo yatalindima maeneo ya Lugoba na kuishia Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

  Akiongea na wanahabri Leo,Rais wa Taasisi ya Automobile Association Tanzania (AAT) ambaye ndiye kiongozi aliyeandaa mashindano hayo,Nizar Jivan amenena kuwa mashindano hayo ya 16 Afrika yatajumuisha madereva 15 kutoka ukanda wa nchi 10 ambayo yatafanyika viwanja vya Bagamoyo.
“Tumejipanga na mashindano ambayo yatakuwa na wachezaji 15 ambao ni madereva kutoka nchi 9 za Ukanda wa bara la Afrika huku akiipongeza Serikali kwa kupitia Baraza la Michezo nchini kwa ushirikiano mkubwa wanaozidi kutupa bila kuwasahau baadhi ya wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini mashindano haya”amesema Jivan
Hata hivyo Mkurugenzi wa Kampuni ya ORYX ,Sophonie Babo ambao ni wadhamini wakubwa wa mashindano hayo amesema kuwa wataendelea kusaidia mashindano hayo kwani yamekuwa yanamanufaa kwao pamoja na kuitangaza kampuni yao kwani wana miaka minne sasa wakiwa wadhamini.
Aidha Meneja wa Mashindano hayo kutoka AAT,Satinda Bird,amesema kuwa wamejiandaa kwa kushirikiana na wadhamini wamejipanga kwa ulinzi na usalama wa madereva na wananchi utakuwa mkubwa siku hiyo ya mashindano hayo.
“Tumejipanga kwa ulinzi zaidi kwa madereva wetu pamoja na wananchi watakaojitokeza katika mashindano hayo kwani tumekuwa na rekodi nzuri ya mashindano haya hatujawahi kupata ajari tofauti na nchi nyingine ambazo zimekuwa zikifanya mashindano kama yetu”amesema Bird

No comments