Header Ads

Responsive Ads Here

MAONESHO YA SABASABA 2017;MAMLAKA YA UDHIBITI WA UNUNUZI KATIKA SEKTA YA UMMA (PPRA), YATOA ELIMU


Meneja Usimamizi na Utawala wa

Mifumo ya TEHAMA, wa Mamlaka ya Udhibiti
wa Ununuzi katika Sekta ya Umma
(PPRA), Bw.Bernard Ntelya, (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensehni wa PPF, Bw. William Erio, alipotembeela banda la Mamlaka hiyo Julai 2, 2017.

NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA
ya
 Udhibiti
wa Ununuzi katika Sekta ya Umma
, (PPRA), kama zilivyo taasisi nyingine za serikali,
imeweka banda lake kwenye jingo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakatihuuwa
maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya
Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Viongozi
na maafisa wa juu wa serikali wamepata fursa ya kutembelea banda hilo ili kujua
huduma wanazotoa kwenye banda hilo, ambapo maafisa wa PPRA, wamekuwa wakitoa
elimu na kugawa vipeperushi vyenye maeelzo mbalimbali ya kazi za Mamlaka hiyo,
lakini na taarifa zinazoeleza sheria ya manunuzi ya umma na umuhimu wake.
Mamlaka
hiyo imeanzishwa kwa sheria ya manunuzi ya Umma CAP 410 kama ilivyobadilishwa
na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya namba 7 ya mwaka 2011 ambayo inatoa Mamlaka ya
kusimamia manunuzi ya umma kwa taasisi zote za Umma (Serikali), upande wa Tanzania
Bara.
Kwa
mujibu wa maafisa wa PPRA walioko kwenye banda hilo, wanasema, malengo makuu ya
PPRA ni kuhakikisha manunuzi yote kwenye taasisi za umma, yanafanyika kwa usawa katika shindani, uwazi, bila unyanyasaji ili mwisho wa siku watoa huduma watoe
huduma inayolingana na thamani ya fedha wanazolipwa kwa maendeleo ya taifa, (Value for Money).
Aidha
wamesema, PPRA inao wajib u wa kuweka viwango katika mfumo wa manunuzi ya umma
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (upande wa Tanzanai Bara).

Afisa Mwandamizi wa PPRA, Bw. Mcharo Mrutu, (kulia), akimpatia vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za PPRA, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio
Bw. Mrutu, (kulia), akizungumza na Mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mamlaka hiyo
Bw. Ntelya(kulia), akifafanua jambo kwa mwananchi huyu aliyefika kujua shughuli za PPRA

No comments