Header Ads

Responsive Ads Here

MALINZI, MWESIGWA KUPANDISHWA TENA KISUTU LEO


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Simba, Evans Aveva, leo Jumatatu wanatarajia kupanda tena mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi zao zinazoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

Marais hao wanatuhumuiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kutakatisha fedha ambapo wote wapo mahabusu kutokana na kunyimwa dhamana.

Washtakiwa wengine ambao wapo sambamba na kina Malinzi ni pamoja na Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Fedha TFF, Nsiande Isawafo Mwanga pamoja na Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Kesi ya Malinzi na Mwesigwa inasikilizwa chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wibroad Mashauri huku kesi ya kina Aveva na Kaburu ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

No comments