Header Ads

Responsive Ads Here

MAKONDA AKAGUA UJENZI WA WODI YA WAZAZI AMANA


index
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.

Ujenzi wa Wodi hiyo ni unafadhiliwa na Kampuni tanzu ya Mafuta na Saruji ya Amsons Group ambayo imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda kwa kujenga wodi tatu wazazi na watoto kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala ambapo zote zitakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 450.

No comments