Header Ads

Responsive Ads Here

MAGUFULI SHUJAA ATAKUMBUKWA DAIMA NA WANACHONGOLEANI


images
Na Judith Mhina – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kielelezo kwetu na atakumbulwa daima na wana Chongoleani wa kizazi hiki cha sasa na kijacho.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chongoleani Bw. Mbwana Nondo alipofanya mahojiano na Idara ya Habari MAELEZO mapema leo kwa njia ya simu.

Nondo aliendelea kumshukuru Rais Magufuli, kwa kuleta mradi wa “Bomba la Mafuta”  linalojengwa kuanzia Hoima Uganda,  mpaka Tanga katika kijiji cha Chongoleani; “Kwa kweli kwa moyo wa dhati kabisa naomba tumshukuru sana sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutujali wananchi wake na kutuletea neema ya Mradi wa Bomba la Mafuta”.
Aidha, amesisitiza;“Katika maisha yetu wana Chongoleani, hatutaweza kumsahau sisi tuliopo wakati huu na vizazi vijavyo,  daima atakuwa mioyoni mwetu, huyu ni shujaa kwetu. Kwa sasa vijana wengi wamepata matumaini ya maisha yao kuwa bora na wameahidi kujituma na kufanya kazi kwa bidii watakapopata ajira katika mradi husika”.
Akifafanua kuhusu suala la vijana  Mwenyekiti Nondo amesema; “Wana Chongoleani hususan vijana naomba msome kwa bidii kwa wale ambao bado wapo shule na kwa wale walimaliza mafunzo mbalimbali, wanamategemeo makubwa Rais atawapigania wapate ajira. Hii itakuwa kichocheo tosha kwa wale wasio penda shule au elimu waone wivu ili wasome kwa bidii kwa kuwa, elimu ni ufunguo wa maisha.
Vilevile, Nondo aliainisha shughuli za kiuchumi kijijini hapo amesema; “Hapa kijijini tuna idadi ya wavuvi kama 200, Mradi wa bomba la mafuta mpaka sasa haujaelekeza suala lolote kwa upande wa eneo letu kubwa la uchumi ambalo ni uvuvi. Hata hivyo, wavuvi wengi wamejiunga kwenye vikundi ambavyo wanashirikiana katika vikoba, vikundi vina idadi ya watu 15 mpaka 20”.
“Kama viongozi bado tunaendelea kuhamasisha wavuvi waweze kujiunga kwa kuwa kuna fedha za milioni 50 kila kijiji huenda wakanufaika na hizo. Pia, kuna ujio wa  mikopo kwa wavuvi kama ilivyoainishwa kwenye hotuba ya bajeti ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Charles Kizeba”. Amesema Nondo
Amemalizia kwa kuwasihi Watanzania, kwa kusema; “Kwa moyo mkunjufu kabisa tunawaomba Watanzania wote wajue Mradi wa Bomba la Mafuta, ni wetu sote kwa pamoja, nina hakika matunda ya mradi huu tutayapata wote Chongoleani ni  muwakilishi tu kati ya vile vijiji, bomba litakapopita na kwa niaba ya Watanzania wote”.  Tumpe ushirikiano Rais wetu anaitakia mema Tanzania nina hakika tutafika mbali kimaendeleo.
Naye Mtendaji Kata wa Chongoleani Bw Mohamed Salum amesema; Rais Magufuli ametupa zawadi kubwa sana ambayo imeweza kuitangaza Kata ya Chongoleani kimataifa, ujio huu wa mradi wa Bomba la Mafuta umetuletea barabara kitu ambacho ni historia kwa wana Chongoleani.
 “Wananchi wana hamasa kubwa kwa ujio wa mradi huu, mpaka sasa kaya 256 zitahama kupisha mradi, na tayari tuko kwenye maandalizi ya kufungua akaunti kwa wale wote watakaopisha mradi ili walipwe mafao yao, kwa kuingiziwa benki moja kwa moja”.Amesema Salum
Kijiji cha Chongoliani kipo kilometa 23 kutoka Tanga mjini, kina idadi ya watu 4737 kaya 1811 wanawake 2410 wanaume 2327 vijana 1672 , Kijiji kipo pembezoni mwa barabara ya kuelekea Mombasa.

No comments