Header Ads

Responsive Ads Here

LIPULI FC YANASA WACHEZAJI WAWILI TOKA YANGA


omega seme #salehjembe
Wageni wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Lipuli FC imewasajili kwa Mkupuo wachezaji wawili ambao walishawahi kuchezea Yanga ambao ni mshambuliaji Malimi Busungu ambaye amesaini mwaka mmoja pamoja kiungo mshambuliaji Omega Seme ambaye naye mwaka mmoja.

Lipuli Fc iliyochini ya kocha Selemani Matola imeanza usajili wa nguvu kwa ajili ya kukabiliana na Mzunguko wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajia kuanza Agosti 26.
Lipuli toka Iringa msimu ujao itatumia uwanja wake wa Nyumbani wa Samora na imecheza mchezo na Azam Fc na kufungwa magoli 4-0 kabla ya kuzinduka na kuifunga Singida United goli 1-0 yote michezo ya kirafiki.

No comments