Header Ads

Responsive Ads Here

LIHIRU-SHULE ZA AWALI 252 MKOANI PWANI KUNUFAIKA NA MRADI WA ELIMU JUMUISHI


unnamed
Kiongozi wa mradi wa elimu jumuishi ,kutoka shirika la kimataifa la ADD tawi la Tanzania,Victoria Lihiru,akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha ,baada ya kuzindua mradi huo utakaodumu kwa miaka minne kuanzia 2017-2021 lengo likiwa kutambua watoto wenye ulemavu

1
Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la ADD ,tawi la Tanzania,Rose Tesha,akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha baada ya kuzindua mradi wa elimu jumuishi utakaotekelezwa katika halmashauri nne za Mkuranga,Kisarawe,Mji wa Kibaha na wilaya ya Kibaha,2017/2021.(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WANAFUNZI wa shule za awali 252 (chekechea)katika halmashauri nne zilizopo mkoani Pwani,wanatarajia kunufaika na mradi wa kuongeza udahili wa watoto wenye ulemavu katika shule hizo na kuboresha elimu jumuishi .
Aidha mradi huo utafikia wazazi na wajumbe wa serikali za mitaa pamoja na walimu 516 ambao watapatiwa elimu kuhusu haki ya elimu sawa kwa watoto .
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo,kiongozi wa mradi kutoka shirika la kimataifa la ADD,Victoria Lihiru,alisema kati ya shule hizo 252 shule 20 zitakuwa za mfano ambapo utekelezaji utafanyika halmashauri ya Mji wa Kibaha,wilaya ya Kibaha,Mkuranga na Kisarawe .
“Tunatekeleza mradi huu, lengo letu kuu likiwa ni kutambua watoto wenye ulemavu kuanzia majumbani kupitia viongozi wa ngazi za chini,wazazi na walezi kuanzia mwaka 2017-2021 “alisema Victoria.
Alieleza kwamba,mradi huo ni chanya ambao utaweza kuwawezesha watoto wenye ulemavu kupata elimu bora kama walivyo wasio na ulemavu ikiwemo miundombinu rafiki na vifaa mbalimbali.
Victoria alisema, watahakikisha watoto hao wanapata haki  na walimu kutoa elimu iliyo bora na kufundisha kwa weledi.
Alisema kwenye mradi uliopita waligundua changamoto zinazowakumba watoto wenye ulemavu ikiwemo baadhi yao kuanza shule umri ukiwa umeenda kuanzia miaka 10-15 .
Victoria alisema na hata wakifikia katika shule wanazojiunga nazo za msingi na sekondari  kunakuwa hakuna mazingira mazuri ya vifaa visaidizi vinavyowawezesha kusoma ,kujifunzia na kufundishiwa na kutokuwa na vyoo vyao.
Mkurugenzi wa shirika hilo la ADD ,tawi la Tanzania,Rose Tesha,alisema wapo  nchini kwa takriban miaka 20 kwa ajili ya kutetea,fursa na usawa kwa watu wenye ulemavu na kufanya kazi na SHIVYAWATA.
Alielezea kwasasa wanatekeleza miradi ya elimu jumuishi kwa kufanyakazi na wizara ya elimu na TAMISEMI kuboresha elimu .
Hata hivyo,Rose alisema wanatetea pia haki za akinamama na kupambana na vitendo vya ukatili kwa  wasichana walio na ulemavu ambapo wamefanya utafiti na kugundua kati ya akinamama wenye ulemavu wa  akili 10 kati yao tisa wanakuwa wamefanyiwa ukatili wa kingono.
Akizindua mradi huo,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,aliwaagiza wakuu wa wilaya,wahandisi na wakurugenzi wa halmashauri mkoani hapo,kuhakikisha wanazingatia ujenzi wenye miundombinu rafiki  mashuleni .
Alisema miundombinu ya madarasa ,vyoo katika shule nyingi haijazingatia usawa baina ya watoto wenye ulemavu na wengine na kusababisha kusoma kwa shida.
Mhandisi Ndikilo ,alisema atafanya ziara ya kushtukiza mashuleni ili kukagua miundombinu na endapo atabaini haijaboreshwa atachukua hatua kwa walimu wakuu .
Anawataka watumishi wa idara ya elimu wawe bega kwa bega na taasisi zinazojihusisha kukabiliana na  changamoto za elimu kama shirika la kimataifa la ADD.

No comments