Header Ads

Responsive Ads Here

LAPF YACHUKUA USHINDI WA KWANZA KIPENGELE CHA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NA BIMA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM


JAMES1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhi ngao ya ushindi wa kwanza Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF huku akiwa na furaha   baada ya shirika hilo kupata ushindi wa kwanza kwa makampuni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Bima  wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE)  yanayoendelea  kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila mwaka kuanzia tarehe 1 mwezi Julai, Kutoka kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage.

JAMES2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi ngao ya ushindi  wa kwanza kwa Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe  baada ya kupata ushindi wa kwanza kwa kipengele cha  Mifuko ya Jamii pamoja na Bima  katika ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje TANTRADE  yanayoendelea  kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila mwaka kuanzia tarehe 1 mwezi Julai, Kutoka kulia wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya (TANTRADE) Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage.
JAMES3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo.
JAMES4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akitembelea mabanda mbalimbali mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa maonyesho hayo wakati alipoyazindua rasmi siku ya jumamosi iliyopita.
JAMES5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maonyesho hayo wakati wa uzinduzi siku ya jumamosi iliyopita.
JAMES6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiondoka kwenye viwanja vya Sabasaba mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi na kuyafungua rasmi maonyesho hayo siku ya jumamosi iliyopita.

No comments