Header Ads

Responsive Ads Here

KIPA WA SERENGETI BOYS ASAINI YANGA MIAKA MITANO

Mabingwa wa kihistori wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya Yanga imeingia mkataba na golikipa wa timu ya Taifa Ramadhani Kabwili wa Miaka Mitano.

Kabwili atakuwa golikipa namba tatu wa mabingwa hao akiwa chini ya wandamizi Youthe Rostand aliyesajiliwa toka timu ya African Lyon iliyoshuka daraja na Beno Kakolonya huku Yanga ikiachana na Ally Mustaf ‘Bethez’aliyejiunga na Singida United pamoja na Dida anayekwenda Afrika Kusini kucheza soka la kulipwa .
 Kabwili mwenye umri wa miaka 17 akikuzwa vyema na kikosi cha Yanga B na timu ya Serengeti boys. Wakati huohuo katibu mkuu wa Yanga SC ametoa taarifa kwa klabu hiyo kuondoka kesho kuelekea Morogoro kwa kambi ya siku 10 kabla ya kurudi jijini Dar es salaam kwa mechi za kirafiki wakianza na Singida United tarehe 5 August.

No comments