Header Ads

Responsive Ads Here

KIKAO CHA WAZI CHA KUTOA MAONI DHAMIRA YA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NCHINI


nembo 3_thumb[1]
Mwaka jana Serikali ilitangaza dhamira ya kupiga marufuku ya kuzalisha, kuuza, kusambaza, uingizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa nchini kutokana na uchafuzi wa mazingira. Kwa kuwa hatua hiyo ni kubwa, Serikali imeamua kuwashirikisha wadau na wananchi ili kupata maoni yao. Kwahiyo, wananchi wote wanaotaka kutoa maoni kuhusiana na hatua hiyo wanakaribishwa katika mkutano wa wazi wa kupokea maoni utakaofanyika siku ya Jumamosi  tarehe 22 mwezi  Julai 2017 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.  Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na utahudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mhe.  January Makamba (MB). Karibuni wote mtoe maoni na sauti yenu isikike.

  Imetolewa na
 Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais,
S.L.P. 5380,
11406 Dar es Salaam.
Barua Pepe: km@vpo.go.tz
Tovuti: www.vpo.go

No comments