Header Ads

Responsive Ads Here

KESI YA KUDAIWA KUVUNJA UKUTA WA KITUO CHA YATIMA YAUNGURUMA ARUSHA.

Arusha,
Kesi ya kudaiwa kuvunja ukuta wa kituo cha yatima cha Huruma Vision Tanzania kilichopo kata ya Sokon I jijini Arusha inayowakabili wakazi tisa wa kata hiyo akiwemo diwani mstaafu wa kata hiyo,Michael Kivuyo imeunguruma jana katika mahakama ya baraza la ardhi na nyumba mkoani Arusha.
 
Katika kesi hiyo ya uharibifu wa mali nambari 147 ya mwaka 2002 shahidi wa tano ,Lesikar Siyatoi ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa mtaa wa Muriet alitoa ushahidi jana mahakamani hapo jana na kusema kwamba mnamo   Julai 11 mwaka 2002  katika kikao cha wananchi kata ya Sokon I alilazimika kupanda pikipiki na kukimbia ili kuokoa usalama wa maisha yake .
 
Akiwasilisha ushahidi wake mbele ya mwenyekiti wa baraza hilo,Fadhili Mdachi shahidi huyo alisema ya kwamba wakati wakiwa  katika kikao hicho  kilichoitishwa kujadili sakata la ukuta huo  baada ya wananchi kumwona diwani mstaafu wa kata hiyo Kivuyo waliamka na kuanza kufanya fujo.
 
Shahidi huyo aliileza mahakama hiyo kwamba mnamo mwaka 2009 akiwa mwenyekiti wa mtaa huo aliitwa na wananchi na kuelezwa kwamba uongozi wa kituo cha Huruma Vision Tanzania ulifunga njia ya kutoka kwa Mromboo kuelekea Mkonoo.
 
Shahidi huyo alisema kwamba mara baada ya kupokea taarifa hizo aliuzuia uongozi wa kituo hicho kutofunga njia jambo walilolipokea kwa mikono miwili ambapo aliitisha kikao cha ujirani mwema ambacho kilihudhuriwa na diwani mstaafu wa kata hiyo,(Kivuyo.)
 
Hatahivyo,shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kwamba katika kikao hicho wananchi walieleza kwamba walitoa eneo la ukubwa wa jumla za ekari 2 na sio 13 na yeye ndipo alipowajibu kwamba mgogoro anaoujua ni kuhusu habari ya kufungua njia na sio ekari za eneo la ardhi walilodai.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi oktoba 24 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka unatarajia kufunga ushahidi wake ambapo shahidi  wa sita anatarajia kuwasilisha ushahidi wake huku upande wa washtakiwa ukitarajia kuanza kutoa utetezi wake mnamo  Novemba 8 mwaka huu.
 
Katika kesi hiyo mkurugenzi wa kituo cha Huruma Vision Tanzania,Godliva Rugumamu  mnamo mwaka 2002 alifungua kesi mbele ya mahakama hiyo akiiomba mahakama hiyo itamke kwamba yeye ndiye mmiliki wa eneo alilopewa na uongozi wa serikali ya kijiji kujenga ukuta huo .
 
Mbali na madai hayo pia mkurugenzi huyo ameiomba mahakama hiyo iamuru alipwe zaidi ya kiasi cha sh,49 milioni kama fidia ya hasara ya ukuta unaodaiwa kuvunjwa na wananchi waliovamia.

No comments