Header Ads

Responsive Ads Here

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA, JAJI MKUU WATEMBELEA BANDA LA WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.


unnamed
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (katikati) akimueleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,             Dkt. Mpoki Ulisubisya (kulia) kazi zinazofanyika kwenye Maabara zilizopo chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali mara baada ya Katibu Mkuu kutembelea Banda la Wakala kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

1
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (katikati) akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (kulia) takwimu za kesi mbalimbali ambazo wachunguzi wa maabara wa Wakala wameweza kuhudhuria kwa kipindi cha Mwaka wa fedha ulioisha baada ya Katibu Mkuu kutembelea Banda la Wakala. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba vya Binadamu, Bw. David Elias.
2
Mtumishi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bw. Emanuel Lewanga (kulia) akimuonesha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma (kushoto) picha za mimiea mbalimbali ambayo hutumika katika kutengenezea dawa za kulevya kama Bangi, Heroin na cocaine baada ya Jaji Mkuu kutembelea Banda la Wakala kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
3
Mtumishi wa Wakala, Bw. Adam Mbugi (kushoto) akimfahamisha mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala shughuli mbalimbali zinazofanywa na Maabara zilizopo chini ya Ofisi Mkemia Mkuu wa Serikali kwa lengo la kusaidia kulinda Afya za Binadamu na Mazingira pia masuala ya Jinai ambayo uwasilishwa kwa ajili ya uchunguzi ili kuhakikisha haki inatendeka kwenye maamuzi ya Kisheria Mahakamani.

No comments