Header Ads

Responsive Ads Here

KARIBU BANDA LA WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI SABA SABA – JAKAYA KIKWETE TENT.


unnamed
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele (kulia) akimsikiliza Afisa wa Polisi aliyetembelea Banda la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuweza kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Maabara zilizopo chini ya Ofisi yake kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya  Saba Saba, Dar es Salaam.

1
Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Bi. Everlight Matinga (wa pili kulia) akimfahamisha mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali huduma zinazotolewa na Maabara za Wakala kuanzia Makao Makuu na Kanda zake Sitazilizoko kwenye Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dar es Salaam, Mtwara na Dodoma.
2
Mtumishi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bi. Lulu Kiwia (kulia) akimueleza mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala huduma zinazotolewa na Maabara ambazo zinahusiana na maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida pia huduma ambazo Wakala inatoa moja kwa moja katika kutekeleza majukumu yake kwa Serikali.
3
Kaimu Meneja wa Masoko na Huduma kwa Wateja, Bw. Cletus Mnzava (wa pili kulia) akimfahamisha mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala shughuli mbalimbali zinazofanywa na kuratibiwa na Maabara zilizoko chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kushoto ni Mtumishi wa Wakala, Bw. Sabas Mandari, akisikiliza.

No comments