Header Ads

Responsive Ads Here

KANISA LAANDA SEMINA YA KUWANOA WANANDOA NA KUTOA VYETI BAADA YA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM


15
Na salesi Malula
Kanisala Tanzania Assemblies of God (Victory Christian Centre VCC) chini ya Mchungaji kiongozi  Dk.Huruma Nkone kwa muda wa mwezi Julai wote kila Jumamosi limeandaa semina kabambe kwa ajili ya kuendesha semina maalumu ya familia na ndoa.

Mafunzo hayo yanafanyika kila jumamosi tar 1,8,15 na 22 julai saa 2:30 – 4:00 asubuhi katika ukumbi wa kanisa hilo lililopo Mbezi Beach A barabara ya Mwaikibaki kilimani close ambapo mafunzo maalumu kwa ajili ya wanandoa yataendeshwa kwa muda wa wiki nne na wahitimu kukabidhiwa vyeti maalumu vinavyotambua ushiriki wa semina hiyo ya kipekee ambayo imedhamini wana kanisa hilo.
Katika semina hiyo itakayokua ikianza asubuhi imeshirikisha wataalamu mbalimbali waliobobea katika mafundisho ya masuala ya ndoa ambap watachambua kwa kina changamoto mbalimbali zinazowakabili wanandoa katika familia zao.
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Dk Huruma Nkone ambaye ndiye mwenyeji wa semina hiyo ya wiki nne aliwataja wenyeji hao kuwa ni Mchungaji Joyce Nkone,mchungaji Halamela Gabriel na mchungaji Samweli Kamangwa Bwana na Bibi Charles Sumbwe,Dk.Chrismauki.
Akichanganua alisema jumamosi ya tarehe 1,8,15 na 22 julai kutakua na shule ya ndoa kwa wanandoa,ambapo washiriki wote watakaohudhuria wiki zote hizo watapewa cheti maalumu cha ushiriki kwani mafunzo haya ni muhimu yatawasaidia watu wengi na hakuna udhehebuni mafunzo ya watu wote bila kujali utofauti wa Imani zaoa lisistiza.
Mara baada ya kuhudhuria mafunzo hayo yanayotolewa bure wiki ya mwisho yatarehe 28 Julai kutakua na dhifa maalumu ya chakula kwa ajili ya wanandoa pamoja na kuwapa vyeti vya ushiriki na naamini mafunzo hayo yatawasaidia wananchi wengi na kuishimaisha bora katika familia zao.
Akihitimisha alisema kwa wale ambao hawana usafiri wao binafsi Kanisa limeandaa usafiri maalumu kutoka makumbusho mwenge na bunju na hakuna kiingilio chochote katika semina hiyo ni bure kabisa.
Kadhalika Jumamosi zote za mwezi Julai saa 4:30 asubuhi-6:30 mchana kutakuwa na ibada za maombi na maombezi kwa wat uwote, wanandoa, vijana, watoto, wazee. Vifungo vya kiukoo na familia vita vunjwa katika ibada hizi.
Na hitimisho la mwezi huuwa familia itakuwa Jumapili tarehe 30 Julai kwenye ibada maalumu ya familia saa 2:00 asubuhi hadi 7 mchana.
Niwaombe wakazi wa jiji la Dar essalaam,na vitongoji vyake kuhudhuri asemina hii muhimu inayoweza kuibadilisha ndoa na kuwa bora Zaidi.
Mawasiliano: 0762441719/0714503638
Facebook: Victory Christian Centre
Instagram: vcctmbezibeach

No comments