Header Ads

Responsive Ads Here

JAFO:TUNATAKA MADARAJA BORA


jafo daraja (1)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akimsikiliza kwa makini Mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Twangoma.

jafo daraja (2)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisikiliza maelezo ya Wakandarasi wanaojenga daraja la Twangoma wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo.
jafo daraja (3)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisikiliza maelezo ya Wakandarasi wanaojenga daraja la Twangoma wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo.
jafo daraja (4)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa ameambatana na Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu katika ukaguzi wa ujenzi wa daraja la Twagomba.
jafo daraja (5)jafo daraja (6)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa ameambatana na Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu katika ukaguzi wa ujenzi wa daraja la Twagomba.
jafo daraja (7)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo katika ukaguzi wa daraja la Twangoma.
jafo daraja (8)
Wajenzi wa daraja la Twagoma wakiendelea na shughuli ya ujenzi.
………………………………………………………………….
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wanaojenga Daraja kubwa la Twangoma linalounganisha  Twangoma na Mbagala kulijenga Daraja hilo kwa ubora unaotarajiwa. 
 Naibu Waziri huyo aliyasema hayo leo alipokuwa anakagua utekelezaji wa maagizo yake alipotembelea eneo hilo mnamo mwezi April mwaka huu.
 Maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kuagiza ujenzi wa daraja hilo uanze mara moja kwani ofisi ya Rais Tamisemi imeshatenga fedha zote za daraja hilo chini ya mradi wa Dar es salaam Metropolitant Development Project (DMDP).
 Akiwa katika ziara yake leo, Jafo amewataka wakandarasi hao kujenga daraja hilo kwa viwango vinavyotakiwa kwa kutumia malighafi ikiwemo nondo zenye ubora unaohitajika.
 Naibu Waziri Jafo amebainisha kuna baadhi ya majengo ambayo yamekuwa yakipomoromoka kutokana na utumiaji wa nondo zisizo na Ubora.
 Aidha Jafo ameridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo kubwa ambapo mradi huo pamoja na barabara yake inayounganisha Twangoma na Mbagala unatarajiwa kugharimu zaidi ya sh.Bilioni 21.
 Naye,Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa ufuatiliaji wa maagizo yake na ameahidi yeye na viongozi wenzake watasimamia mradi huo kwa karibu ili ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

No comments