Header Ads

Responsive Ads Here

JAFO AWAPA MATUMAINI WATAALAM WA AFYA BAHI


JK
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha Afya Bahi baada ya kutembelea kituo hicho.


NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapa matumaini wataalam wa sekta ya Afya wilayani Bahi kuwa serikali ipo katika mpango wa kukarabati kituo cha afya Bahi ili kiweze kituo huduma bora za afya tofauti na ilivyo sasa. 
 Akizungumza na wataalam hao leo katika ziara yake wilayani humo, Jafo alisema wilaya hiyo haina hospitali ya wilaya kwasasa hivyo serikali inafanya jitihada za kuboresha utoaji huduma katika Kituo hicho.
 “Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli imedhamiria kuanza ujenzi wa chumba cha upasuaji na kukarabati majengo mengine ili wananchi wa Bahi waweze kupata huduma ya upasuaji,”amesema Jafo
 Ameeleza kuwa kwasasa wananchi hao wanalazimika kufuata huduma za upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma iliyopo umbali wa zaidi ya kilometa 60.
 Naibu Waziri Jafo amewaambia wataalam hao kuwa ujenzi huo unatarajiwa kuanza wakati wowote ili kuwaondolea adha wananchi wa eneo hilo.

No comments