Header Ads

Responsive Ads Here

JAFO AHIMIZA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO YA WANACHAMA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.


JF (1)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF katika mpango wa hiyari leo baada ya kufungua semina kwa ajili ya wastaafu watarajiwa inayoendelea mkoni Dodoma.

JF (2)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo (kulia) akimkabidhi Bi Neema Muro (kushoto)fomu ya kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii katika mpango wa hiyari hapo mara baada ya kuijaza katika ufunguzi wa semina kwa ajili ya wastaafu watarajiwa inayoendelea mkoni Dodoma.
JF (3)
Mzee mstaafu akitoa ushuhuda kwa kundi la wanachama wa mfuko wa PSPF wanaotarajiwa kustaafu katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Dodoma.
JF (4)
Washiriki wa semina hiyo katika matukio mbalimbali
JF (5)
Washiriki wa semina hiyo katika matukio mbalimbali
JF (6)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akihutubia mamia ya wanachama wa mfuko wa PSPF ambao wanatarajiwa kustaafu miaka michache ijayo.
JF (7)
Mkurugenzi wa mfuko wa PSPF Adam Mayingu akiongea na wanachama wa mfuko huo  katika semina inayoendelea mkoani Dodoma ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wanachama hao kujiandaa na masiha yao baada ya kustaafu.
………………………………………………………………………………..
Naibu waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewahimiza waajiri wote kuwasilisha michango ya waajiriwa wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kustaafu.
 Jafo aliyasema hayo alipokuwa mgeni Rasmi katika semina ya wafanyakazi wanaotarajiwa kustaafu kipindi cha miaka miwili ijayo ndani ya mkoa wa Dodoma. 
 Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa kijasiriamali wastaafu hao watarajiwa ili watakapopata fedha zao za kustaafu waziwekeze katika shughuli muhimu za kiuchumi ili wasije wakawa ombaomba kwa kushindwa kuzitumia fedha hizo ipasavyo. 
 Katika mkutano huo, Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia mafao yao.
 Kadhalika, amewasihi wastaafu hao watarajiwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kujihusisha katika kilimo na ufugaji wa kisasa ili waweze kuwa na uchumi imara.
 Naye, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Adam Mayingu, amebainisha kuwa mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika kipindi cha 2017/18 ambazo ni mafao ya watumishi 9552 wanaojiandaa kustaafu katika kipindi cha kati ya Mwaka huu na mwakani.

No comments