Header Ads

Responsive Ads Here

IMU YA EVERTON YA UINGEREZA YAFADHILI MATIBABU YA WAGONJWA WA MABUSHA NA MATENDE TANZANIA


01
Mtangazaji wa Televisheni ya Everton, Darren Griffiths,   akizungumza na wagonjwa waliotibiwa na kufanyiwa upasuaji wa Mabusha na Matende nchini Tanzania wakati walipokutana katika hoteli ya Seacliff jijini Dar es Saalam Timu  hiyo ipo nchini kwa mchezo mmoja wa kati yao na timu ya Gor Mahia ya Kenya ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Timu ya Everton imekuwa ikifadhili matibabu ya wagonjwa wa Mabusha na Matende kupitia Taasisi ya LSTM Surppoting Tanzania Program ya Liverpool nchini Uingereza kupitia Mpanga wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.
1
Mratibu wa  Mpango wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele Dk. Upendo Mwingira  akitambulisha wageni kutoka timu ya Everton na baadhi ya wagonjwa waliotibiwa kupitia mpango huo kwa ufadhili wa timu hiyo.
2
Meneja Mradi wa Taasisi ya LSTM Hayley Mebalsone  akizungumzia kuhusu ufadhili wa timu ya Everton kwa Tanzania katika mpango huo wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Mabusha na Matende.
3
Baadhi ya wagonjwa waliopata tiba na wanaoendelea kupata tima wakiwa katika hafla hiyo.
4
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Vida Mmbaga akiwashukuru wachezaji wa Everton na wagonjwa kwa kukutana na kushiriki katika hafla hiyo ambayo imewafanya kufahamiana na kujua kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi ya (LSTM) kwa pamoja na timu ya Everton.
  6
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman na Mtangazaji wa Televisheni ya Everton Darren Griffiths aliyeinama wakigawa zawadi kwa wagonjwa walitibiwa na wanaoendelea kutibiwa ugonjwa wa Mabusha na Matende wakati walipokutana kwenye hoteli ya Seacliff jijini Dar es salaa. leo.
7
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman na Mtangazaji wa Televisheni ya Everton Darren Griffiths Graham Stuart pamoja na viongozi kutoka wizara ya Afya pamoja na wagonjwa waliopata matibabu na wanaoendelea kupata matibabu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
8

No comments