Header Ads

Responsive Ads Here

HALMASHAURI JIJI LA ARUSHA YAZINDUA KANUNI MPYA


calist-Lazaro
Baraza la Madiwani Jiji la Arusha linezindua kanuni mpya zitakazoongoza baraza hilo kwa mujibu wa sheria. 
Aidha baraza hilo linachagua Naibu Meya ili aweze kuongoza baraza hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja huku madiwani wawili wanawania nafasi hiyo kuwa ni Abdulrasul Tojo Diwani wa Kata ya Mjini Kati huku aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji hilo,  Viola Lendikoki akitetea nafasi yake. 

Akizindua kanuni hizo mpya, Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema kanuni hizo ndizo zitakazoongoza madiwani hao kuendesha vikao vyao vya baraza hilo la madiwani pia alisisitiza madiwani hao kuzingatia kanuni hizo zilizosomwa na mwanasheria wa Jiji la Arusha. 

Baada ya uzinduzi wa sheria hizo, wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu waliwasilisha taarifa za kamati zao za ikiwemo Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya, Kamati ya Mipango miji, Mazingira na Ujenzi  sanjari na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi. 

Akiwasilisha taarifa ya ripoti ya kamati ya Uchumi, Afya na Elimu na Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita alisema wamehamasisha kaya 2,157 kujiunga na Tika  ikiwemo ununuzi wa madawati 1,800 katika shule za msingi 

Huku Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji Ally Bananga akiwasilisha ripoti yake alisema ufinyu wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 umepelekea baadhi ya maeneo kushindwa kuboresha mazingira pia mgao wa maji AUWSA unafanya bustani za mizunguuko kutokuwa kijani cha kuvutia ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuchimba visima kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji. 

Awali Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia aliwapongeza madiwani hao kufikisha mwaka mmoja ikiwemo kutekeleza na kusimamia shughuli mbalimbali za Jiji la Arusha sanjari na kushirikiana na wataalam wa Jiji katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unavuka leo. 

Baraza hilo la madiwani limemaliza mwaka mmoja jana huku wabunge wa Viti maalum Mkoa wa Arusha, Catherine Magige kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Joyce Mukya wakihudhuria baraza hilo sambamba na makatibu wa vyama mbalimbali vya siasa pamoja na wanachi wa Jiji la Arusha. 

No comments