Header Ads

Responsive Ads Here

GROBAL EDUCATION LIK LIMITED YAPUNGUZA WIMBI LA WANAFUNZI WANAOSOMA NJE YA NCHI KUACHA VYUO NA KUKIMBILIA BIASHARA


1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ngao ya ushindi Bi. Zakia Nassor Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited ya jijini Dar es salaam kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa udhamini wa maonyesho ya baisaha yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Kulia anayeshuhudia ni Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage

2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimshuhudia Bi. Zakia Nassor  Mkurugenzi wa Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limitedi ya jijini Dar es salaam wakati akimshukuru Mh. Waziri Charles Mwijage baada ya kukabidhiwa ngao yake ya ushindi kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa udhamini wa maonyesho ya baisaha yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE Bw. Christopher Chiza.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimshuhudia Bi. Zakia Nassor  Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited  ya jijini Dar es salaam wakati akishuka jukwaani baada ya  kukabidhiwa ngao yake ya ushindi kama ishara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje TANTRADE kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa udhamini wa maonyesho ya biashara  yanayoendelea kwa siku 14 kwenye Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na Mwenyekiti wa Bodi ya TANTRADE Bw. Christopher Chiza na Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bi. Zakia Nassor  Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye viwanja vya maonyesho vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar essalaam leo.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Bi. Zakia Nassor  Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited wakati alipotembelea banda hilo leo kulia ni Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mh.Charles Mwijage
7
Bi. Zakia Nassor  Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited akizungumza na Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL aliyetembelea katika banda hilo, Kampuni ya Grobal Education Link Limited imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo kwa mhandisi mmoja  wa shirika hilo katika nchi ya China ambako amekwenda kuchukua ujuzu zaidi katika uhandisi wa Ndege
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na msafara wake akiingia kwenye banda la Grobal Education Link Limited wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
………………………………………………………………………………………
Bi. Zakia Nassor Mkurugenzi wa  Utawala Kampuni ya Grobal Education Link Limited ya jijini Dar es salaam inayojishughulisha na kuwatafutia vyuo nje ya nchi wanafunzi wa kitanzania  amesema kampuni yake imewezesha wanafunzi kusoma kwa bidii na wazazi kutopoteza fedha tena baada ya kuweka udhibiti kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kupitia kampuni yao.
Bi. Zakia Nassor ameyasema hayo wakati akizungumza na mtandao wa  Fullshangwe kwenye maonyesho ya 41  ya biashara yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) na kufanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam  kila mwaka kuanzia Julai 1.
Amesema Kampuni yao inatoa ushauri kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma katika vyuo vya nje ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa  wazazi pia ili kujua watoto wao wanaweza kusoma  kozi gani  kulingana na soko lililopo kwenye ajira ikiwa ni pamoja na kujua viwango vya vyuo wanavyokwenda kusoma.
Ameongeza kwamba Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali kama vile TCU, NECTA na NACTE ili kukidhi vigezo vya wanafunzi wenye sifa kujiunga na vyuo hivyo  katika suala zima la vyeti feki jambo ambalo linaokoa fedha wanazotoa wazazi ili kulipia ada na kuwafanya wanafunzi wasome vyuo hivyo huku wakiwa na uhakika na vyeti na taaluma zao mara watakapomaliza vyuo na kurudi nyumbani tayari  kuingia katika soko la ajira.
Kampuni hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha inawafuatilia wanafunzi katika mahudhurio na ufaulu wa mitihani yao wawapo vyuoni  ili kumrahisishia mzazi kufuatilia maendeleo ya mtoto wake awapo chuoni ambapo  kampuni hiyo imeweka mawasiliano madhubuti  na  ya moja kwa moja na kati yake na vyuo wanavyosoma watoto nje ya nchi ili kurahisisha wazazi kujua maendeleo ya watoto wao.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la wanafunzi wengi kutomaliza masomo yao na kujiingiza katika shughuli za biashara au kuacha masomo huku wazazi wakiamini watoto wako shuleni. kumbe hakuna kinachoendelea, matokeo yake wazazi wamekuwa wakipoteza fedha huku watoto wakishindwa kufikia malengo kutokana na  kufeli mitihani yao kwa sababu hakukuwa na utaratibu wa kumfuatilia mwanafunzi akiwa chuoni
Kampuni hiyo imekuwa ikipeleka wanafunzi wa kitanzania katika vyuo mbalimbali nje ya nchi ambavyo viko katika nchi za Uingereza, Marekani, Canada, Australia, Ukrane, India, Malaysia, China na Afrika Kusini.

No comments