Header Ads

Responsive Ads Here

GLOBAL EDUCATION LINK YAFANYA UDAHILI WA PAPO KWA PAPO KWA VYUO VIKUU VYA NJE


 Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel wa (kwanza kushoto) akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

 Afisa Masoko wa Global Education Link (GEL) Damaricy Peter wa (kwanza kushoto) akiwapa maelekezo  wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Hati ya Kusafiria Passport , Abdul Milanzi akimsainisha fomu ya hati ya kusafiria mteja wa Global Education Link GEL  leo  katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional, Love Kumas (kulia) akizungumza na mteja katika ofisi za  Global Education Link (GEL) leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
…………………………………………………………………………..
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baada ya Matokeo ya Kidato cha Sita , Global Education Link (GEL) ambao ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa  wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu vya nje udahili ni papo kwa papo  na  vyuo hivyo viko wazi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi  Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema  katika azma ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda, inahitaji rasilimali watu  ya kutosha  ambao  ndio watasukuma gurudumu hilo la  viwanda na ujuzi upo katika vyuo vya nje ambapo nchi zenye vyuo vina uatajiri wa viwanda.
Mollel amesema kuwa vyuo ambavyo anashirikiana na vina uwezo wa kutosha  katika uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta  ya  viwanda.
Amesema kuwa wazazi wanaotaka kupeleka wanafunzi katika vyuo vikuu vya nje  hawatajutia kutokana na mazingira wanayokwenda kusoma huko.
Mollel amesema kuwa  wazazi na wanafunzi wafike katika ofisi zao  ziko katika mikoa ya Dar es Salaam viwanja vya Saba saba , Dodoma , Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Arusha  pamoja na nchi  ya Zambia.
Amesema kuwa mwanafunzi atayekuwa anapitia katika wakala hiyo atapata uangalizi kwa muda wote masomo yake katika kuhakikisha mzazi kile anachokifanya kwa kijana wake hawezi kujutia.
Mollel amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanaweza kufika katika ofisi zao kwa maelezo na jinsi kuwafanyia udahili wa papo kwa papo.

No comments