Header Ads

Responsive Ads Here

GARI LATUMBUKIA MTO WAMI NA KUUA WATU WAWILI

Picha hii ya mtandao inaonyesha moja ya ajali zilizowahi kutokea katika mto huo.

MADEREVA wawili wa kampuni ya Usangu Logistics wamekufa baada ya gari la
 mizigo walilokuwa wakisafi ri nalo kutumbukia katika Mto Wami uliopo Chalinze, 
wilayani Bagamoyo.

Akizungumza jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana 
alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa saa 7:00 kuamkia jana. Gari aina ya Scania lenye 
namba za  usajili T857 ARP lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Arushalilikatika 
breki na kugonga kingo za mto na kutumbukia mtoni.

Dereva aliyekuwa anaendesha gari hadi linatumbukia mtoni ametajwa kuwa ni 
Yahaya Karim anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 na 35. Alisema jina na mtu 
mwingine ambaye pia ni dereva, halikufahamika mara moja.

Matukio ya ajali yamekuwa mengi nchini. Kwa mujibu wa jeshi la polisi kitengo 
cha usalama barabarani, hadi Novemba mwaka jana watanzania 2,994 walikufa kwa 
ajali mbalimbali za barabarani za mabasi, malori, magari madogo, bajaji na bodaboda.

Ili kukabiliana na ajali hizo, jeshi hilo limekuwa likiendesha operesheni katika 
barabara zote kuu nchini kwa mfano kutumia tochi kukamata madereva wanaoendesha 
kwa mwendokasi  au kwa uzembe.

Pia limekuwa likiwataka wananchi kushirikiana na polisi kuchukua hatua 
mbalimbali za kudhibiti ajali kwa mfano kutoa taarifa mara kwa mara wakiwa safarini, wanapobaini madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani. Aidha limekuwa 
likihimiza wananchi kutoa ripoti katika vituo vya polisi juu ya madereva wanaofanya 
makosa.

IMEANDIKWA NA JOHN GAGARINI, KIBAHA

No comments