Header Ads

Responsive Ads Here

FIFA YARIDHISHWA NA TAARIFA YA VIONGOZI WA MUDA TFF


Baada ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kuelezwa kwamba italeta wawakilishi wake nchini kwa lengo la kufuatilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), sasa mpango huo umefutwa baada ya kukubaliana na taarifa ilizopewa na uongozi wa muda wa shirikisho la soka nchini.
Taarifa za Fifa kusitisha mpango wake wa kuja nchini kufuatilia mchakato huo zimetolewa na Kaimu Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye amesema imetokana na mazungumzo baina yao pamoja na taarifa waliyoituma kwenye shirikisho hilo linaloongoza soka duniani.
Katika taarifa yake, Karia alisema baada ya Fifa kuelezwa kwa kina kila kitu kinachoendelea kupitia maelezo ya viongozi wa TFF, waliridhishwa na mazungumzo hayo yaliyofanyika kabla ya kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo mapema leo Jumanne.
Mbali na Fifa kuridhika na maelezo ya TFF pia shirikisho hilo limekubaliana na kikao hicho cha kamati ya utendaji kilichotarajiwa kufanyika leo Jumanne ikiwa ni pamoja na kutoa baraka zao na kuitakia heri kamati hiyo.

No comments