Header Ads

Responsive Ads Here

FAO YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI


Na Mahmoud Ahmad Arusha

SHIRIKA la chakula Ulimwenguni, FAO, limeahidi  kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wakulima wanazalisha chakula cha kutosheleza na hivyo kuondoa tatizo la uhaba wa chakula kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.

Mwakilishi wa FAO ,Fred Caferody,ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu kwenye siku ya wakulima wa mazao mchanganyiko ya chakula na biashara kutoka mikoa mbalimbali nchini yaliyofanyika kwenye viwanja wa taasisi ya utafiti wa mazao, Seliani jijini Arusha.
Amesema FAO, imekuwepo hapa nchini kwa miaka 40 imekuwa ikiandaa sera na program mbalimbali za kilimo na chakula ili kuwezesha wakulima kuzalisha chakula kinachotosheleza mahitaji kwa kushirikiana na serikali na swala la kilimo na chakula ni sehemu ya jukumu lake kuhakikisha hakuna upunfgufu wa chakula nchini.
Kwa upande wake baraza la nafaka la Afrika mashariki, EAGC,limesema litaendelea kushirikiana na vituo vya utafiti wa mazao ya kilimo kwa nchi za afrika mashariki  katika kutafuta masoko ya nje wakulima nchini.
Mkurugenzi wa fedha wa shirika hilo Drollah Ssebagala, amesema baraza la nafaka  litakuwa likiwapatia wakulima taarifa za masoko  kwenye nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia DRC congo, Malawi na Zambia Sudani na Ethiopia
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa utafiti wa mazao nchini kutoka wizara ya Kilimo na Mifugo, Dakta Jackson Nkuba, amesema upo ugonjwa wa Manjano unaoshambulia mahindi  na hilo ni tatizo kubwa hivi sasa serikali kupitia wizara ya kilimo imeweka nguvu kubwa ili kuudhibiti ugonjwa huo.
 Amesema kuwa ugonjwa huo ni tatizo kwa kuwa unashambulia mahindi yakiwa shambani na kunyauka hivyo mkulima anapata hasara .
Amesema kuwa hayo ni maonyesho ya nne ya mnyororo wa mazao ya kilimo kufanyika nchini ni maonyesho muhimu sana na yatapanuliwa katika kanda zingine nchini lengo ni kuwezesha wakulima kupata teknolojia ya kilimo cha biashara kutoka kilimo cha kujikimu .
Hivyo akayataka makampuni ya uzalishaji  wa mbegu bora kutoka kwenye taasisi za utafiti wa mbegu ambayo yataongezeka ili kuwafikia wakulima ili kuwafikia wakulima waweze kuzalisha mazao bora na kulima kilimo cha kibiashara.
 
Akifungua maonyesho hayo Katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega, amesema mpango wan chi katika kilimo ni kuendelea kushirikiana na  baraza la Nafaka la nchi za afrika mashariki,shirika la kilimo na chakula ulimwengini, FAO na wadau wengine
Amewataka watafiti wa mbegu kuhakikisha matokeo ya uutafiti wanazofanya yanawafikia wakulima ili kuweza klkuleta tija vinginecvyo yasiopowafikia walengwa hayawezi kuleta tija kwenuye kilimo.
Amezitaka taasisi zingine binafsi kuongeza ushirikiano na serikali ili kuharakisha maendeleo na upatikanaji wa mbegu bora za mazao aina mbalimbali za mazao.
Amesema uzalishaji mdogo wa mazao unachangiwa na  kilimo kisichozingatia utaalamu ,ukosefu wa masoko mazao kushambiliwa na magonjwa ucheleweshwaji wa pembe jeo  kutokuwepo kwa vikundi vya wakulima miundo mbinu hafifu  ya kuhifadhia mazao na kuendelea na kilimo cha kizamani.
Hivyo akatoa wito kwa wataalamu wa kilimo kuanzisha mashamba darasa kila eneo ili wakulima waweze kupata elimu na kubadilisha mbinu za kilimo kutoka cha kujikimu na kuwa cha kibiashara.
Akawataka viongozi wa vijiji kihakikisha kila kaya inatenga hekari moja yitakayotokana na kilimo cgha mazao yanayotokana na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na hivyo kuharakisha mabadiliko .

No comments