Header Ads

Responsive Ads Here

DKT. PHILIP MPANGO ABAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA DODOMA HAWATUMII IPASAVYO EFDs


IMG_4441
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa na katika mitaa ya mji wa Dodoma alipofanya ziara ya kushitukiza, kukagua matumizi ya mashine za kutolea risiti kwa njia ya kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara wa maduka mjii humo.
IMG_4473
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua mashine ya EFD na risiti ya kieletroniki aliyopewa baada ya kununua bidhaa kwenye moja ya maduka mjini Dodoma, alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua kama wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo mashine hizo.

IMG_4484
Kiongozi wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.
IMG_4500
Mfanyabiashara wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb),  baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka lake na kubaini kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.
IMG_4547
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipitia kwa makini fomu ya makadirio ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika moja ya duka la vipodozi mjini Dodoma wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD’s katika baadhi ya maduka yaliyopo mjini humo.
IMG_4550
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuonya mfanyabishara wa mjini Dodoma, Bw. Isdori Shirima, baada ya kukuta akiuza bidhaa bila kutoa risiti za kielektroniki kwa wateja wake inavyotakiwa na kuagiza Mamlaka ya Mapato mkoani humo kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini kiwango cha ukwepaji kodi cha mfanyabiashara huyo na kumchukulia hatua za kisheria.
IMG_4547
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti ya mteja aliyenunua tanki la kuhifadhia maji katika moja ya duka linalouza vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi kukagua risiti zao ili kubaini kama kiwango kilichoandikwa kinalingana na kiasi kilichoandikwa kwenye risiti.
IMG_4569
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimwelekeza mwananke mmoja aliyemkuta dukani akague risiti yake baada ya kufanya manunuzi kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza ili kubaini namna wafanyabiashara wa maduka mjini humo wanavyotumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti.
IMG_4580
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuagiza Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Ngaka Magere, kumkutanisha na mawakala wanaosambaza mashine za kieletroniki za kutolea risiti mkoani humo baada ya kutoridhishwa na huduma zao
IMG_4585
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo ya matumizi ya mashine za kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi wa Kituo kimoja cha  Mafuta mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza kituoni hapo kuangalia matumizi ya mashine hizo.
IMG_4594
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti na kupata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Kituo cha Mafuta cha ORYX mjini Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin, alipofanya ziara ya kushitukiza kuangalia kama vituo vya mafuta mjini humo vimefungwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti kwa wateja wao.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
……………………..
BENNY MWAIPAJA, DODOMA
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika mitaa ya mji wa Dodoma na kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatumii ipasavyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi ya Serikali-EFDs na kuwaonya wafanyabiashara kote nchini kuacha mchezo huo.
Dkt. Mpango aliyeambatana na baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini-TRA mkoa wa Dodoma amebaini baadhi ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu hawatoi risiti huku wengine wakiandika kiwango kidogo cha fedha kwenye risiti hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara aliyekumbana na mkono wa Waziri Dokta Mpango, ni Bwana ISDORI SHIRIMA ambaye amekiri kufanya makosa ya kutotumia mashine hizi ipasavyo
“naomba unisamehe Mheshimiwa, sitarudia tena unajua sisi vijana tunabangaiza, lakini nimebaini nimefanya makosa” aliomba msamaha Bw. Shirima
Hata hivyo Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA mkoa wa Dodoma, kufanya ukaguzi wa kina wa mahesabu ya mfanyabiashara huyo ili kubaini kiwango cha kodi alichokwepa na kumchukulia hatua stahiki.
Aidha, Dokta Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Dodoma kuwapeleka ofisini kwake mawakala wote mkoani humo wanaosambaza mashine za kieletroniki za kukusanyia mapato EFDs baada ya kubaini kuwa zaidi ya mashine 100 zimeharibika na hazitumiki tangu jana.
“Kuna kitu sikielewi na hakiingii akilini, inakuwaje mashine ziharibike kwa kiwango hicho, mashine 100 kuharibika kwa siku mbili ni nyingi na ina maana nimekosa mapato mengi” alielezea kwa masikitiko Dkt. Mpango.
Aliagiza mawakala wote wanaosambaza ama kuuza mashine hizo wakutane naye ofisini kwake mjini humo ili kubaini tatizo na kuongeza kuwa haiwezekani wafanyabishara walipie mashine hizo zaidi ya mwezi uliopita lakini hawapelekewi hali inayozidi kuikosesha Serikali mapato yake.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamepongeza uamuzi wa Serikali wa kulivalia njuga suala la kodi na kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kutoa risiti wanapouza bidhaa na kudai risiti zenye viwango sahihi vya manunuzi waliyoyafanya ili kuijengea Serikali uwezo wa kuihudumia jamii.
Dokta Mpango ametembelea pia baadhi ya vituo vya mafuta mjini humo na kuwakumbusha wamiliki wote wa vituo vya mafuta kuzingatia agizo la Serikali linalowataka wafunge mashine maalumu za kielektroniki zinazofungwa kwenye pampu za mafuta ndani ya siku 14 ambazo ziko ukingoni.

No comments