Header Ads

Responsive Ads Here

CHINA YAIJENGEA UWEZO IDARA YA FORODHA YA TANZANIA


IMG_4276
Naibu Kamishna wa forodha na Maboresho ya Vihatarishi Hatari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. James Mbunda (Kushoto) na akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong, wakati wa kufungua mafunzo kuhusu Takwimu na kudhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam.

IMG_4279
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Grace Sheshui akiwakaribisha watoa mafunzo ya Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam.
IMG_4293
Naibu Kamishna wa Forodha na Maboresho ya Vihatarishi Hatari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. James Mbunda, akizungumza na  watoa mafunzo ya Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong.
IMG_4318
Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa makini maelezo ya awali ya mafunzo ya kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
IMG_4320
Maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na wengine (kulia) na wakufunzi wa Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha wakisikiliza maelezo ya awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
IMG_4336
Mkufunzi Mkuu wa masuala ya forodha kutoka Chuo cha Forodha cha Shanghai, China, Profesa Sun Hao (kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku 14 ya maafisa wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dae Salaam.
IMG_4359
Naibu Kamishna wa Forodha na Maboresho ya Vihatarishi Hatari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. James Mbunda (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi, pamoja na maafisa wa forodha kutoka TRA, baada ya ufunguzi wa mafunzo ya siku 14 kuhusu masuala ya forodha, katika ukumbi wa Wizara ya fedha na Mipango, Jijini, Dar es Salaam.
IMG_4363
Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong (Kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Grace Sheshui (kulia) wakipeana mkono baada ya ufunguzi wa mafunzo ya masuala ya forodha yanayotolewa na Chuo cha  Forodha cha Shanghai, China, mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

No comments