Header Ads

Responsive Ads Here

CCM PWANI YAMALIZA ZOEZI LA KUCHUKUA FOMU


kixNa Mwamvua Mwinyi,Pwani
Zoezi la uchukuaji fomu kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)2017,mkoani Pwani,limeenda vizuri ambapo wanachama  wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi zilizotangazwa.

Zoezi hilo lilianza rasmi july 2 na kukamilika july 10 na sasa hatua inayosubiriwa itakuwa ni vikao vya mapendekezo kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni.
Katibu wa CCM mkoani Pwani,Anastazia Amas anasema, waliochukua fomu kugombea nafasi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa mkoani humo ni 11 na nafasi ya mwenyekiti mkoa ni wanne.
Wilaya ya Bagamoyo waliojitokea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti ni watatu,Kibaha Mjini ni 11,Kibaha Vijijini waliochukua fomu kwa nafasi hiyo ni watano.
Waliochukua fomu kuwania nafasi ya mwenyekiti wilaya ya Kibiti ni watano,Kisarawe wanne,Mafia kumi,Mkuranga sita na Rufiji wamechukua fomu hiyo wanne.
Nae katibu wa CCM Kibaha Mjini,Abdallah Mdimu ,amebainisha,nafasi ya katibu mwenezi wamejitokeza watu watano,wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya kwa makundi ya UVCCM,UWT na Wazazi wamejitokeza watu 36,ngazi ya mkutano mkuu wa Taifa 30,mkutano mkuu wa mkoa 26 na halmashauri kuu ya CCM ya mkoa wamejitokeza watu 13.
Mdimu ameeleza kwasasa hakukuwa na harufu ya kubebana wala kupanga safu kutokana na elimu waliyoitoa kuanzia ngazi za chini.
Amesema mchakato mzima upo vizuri na anaamini CCM Mjini hapo ,itapata viongozi wenye uchungu na chama,waadilifu,wachapakazi na wawajibikaji.

No comments