Header Ads

Responsive Ads Here

YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP,YAIGONGA TUSKER YA KENYA


unnamed
Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
1
 Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
2
Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) akichuana na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
3
 Yusuph Mhilu wa Yanga akimtoka beki wa Tusker
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga imekuwa timu ya kwanza toka Tanzania kutinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penalti.
Baada ya mchezo wa kwanza uliowakutanisha Singida United dhidi ya AFS Leorpads na vijana wa Hans Van Der Pluijm kutolewa nje kwa njia ya mikwaju ya penalti 5-4
Yanga imeing’oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.
Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung’olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao.
Kwa sasa Yanga wametinga nusu Fainali na watakutana na AFS Leorpads siku ya Alhamis na Fainali ya Michuano hiyo itachezwa siku ya Jumapili Juni 11 na bingwa atacheza na Everton katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam July 13 mwaka huu.

No comments