Header Ads

Responsive Ads Here

YANGA YAAGA MASHINDANO YA SPORTPESA,KUNA UWEZEKANO FAINALI IKAWA DABI YA MASHEMEJI WA KENYA


 Beki wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.

 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan  Katerega, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup
 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah  Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup
 Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC  Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup
 Mshambuliaji wa Yanga Yusuph Mhilu (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup
 Winga wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akimfinya beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup
 Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
 Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup,
 Mhilu akimkalisha beki wa AFC Leopards
…………………………………..
Na.Alex Mathias,Dar es salaam

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Yanga ambao walikuwa wawakilishi pekee wa nchini kwenye Michuano ya SportPesa Super Cup hatimaye nayo imeyaaga mashinadno hayo baada ya kutolewa kwa njia ya Penalti 4-2 hatua ya Nusu Fainali na AFC Leopards toka Kenya.
Watanzania wengi walikuwa wana imani na Yanga kuwa huenda wakaingia Fainali kwa bahati mbaya nao wametolewa na kuwaacha wageni wakitesa kwenye Ardhi ya nyumbani na bingwa wa Michuano hiyo atacheza na timu ya Everton toka Uingereza Julai 13 mwaka huu katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Shukrani za ushindi wa Leopards zimuendee Mlinda Mlango ambaye amepangua penalti mbili za Yanga ya Said Mussa na Said Juma ‘Makapu’ huku akifunga mkwaju wa ushindi kwa kutungua Dida.
Ushindi wa AFC Leopards umewafanya watinge hatua ya Fainali na wanatarajia kukutana na Gor Mahia au Nakuru huku kuna uwezekano Mkubwa dabi ya Mashemeji kukutana Fainali siku ya Jumapili huenda kwa mara ya kwanza Derby ya Kenya kuchezwa nje ya nchi yao yaani Gor Mahia na AFC Leopards.

No comments