Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA MAZUNGUMZO BALOZI WA FINLAND NA UJUMBE WA UBALOZI WA MAREKANI LEO MJINI DODOMA


Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili namna ya kuimarisha sekta ya misitu nchini ikiwemo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mazao ya misitu pamoja na uzalishaji wa nishati mbadala.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka (kulia) ofisini kwake leo mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamezungumza kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika kuendeleza sekta ya Maliasili hususan vita dhidi ujangili, kuongeza idadi ya watalii pamoja na mapato yatokanayo na utalii.
 Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson (katikati) akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimkabidhi Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson majarida mbalimbali yanayozungumzia vivutio vya utalii vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika kikao hicho cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) na Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson leo mjini Dodoma. (PICHA NA HAMZA TEMBA – WMU)

No comments