Header Ads

Responsive Ads Here

Waziri Mhagama azindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana mkoani Iringa


iri1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Mhe Jenista Mhagama amezindua Programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi wa stadi za maisha ya Taifa kwa vijana, Mkoani Iringa mpango ambao utawanufaisha vijana elfu tatu mianne 3,400 mpango  unaogharamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe Mhagama amesema mpango huu ni sehemu ya kuwaandaa vijana ambao watashiriki katika mapinduzi ya viwanda nchi Tanzania na utasaidia kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa kupitia mafunzo ya Uanagenzi, katika nyanja za ujenzi, tehama, ufundi magari, na ushonaji nguo katika mikoa yote nchini Tanzania.
Katika awamu hii ya kwanza, mpango huu unaendeshwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na taasisi ya Wasalesiani wa Don Bosco Tanzania.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Naibu waziri Mhe Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Wabunge kutoka mkoa wa Iringa, na Njombe na Mkuu wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco Africa Mashariki Fr. Simon Asira.

No comments