Header Ads

Responsive Ads Here

WATEJA WAMIMINIKA KWENYE BANDA LA LAPF KATIKA MAONYESHO YA TANTRADE VIWANJA VYA SABASABA BARABARA YA KIRWA JIJINI DAR ES SALAAM


1
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika banda la mfuko huo kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya BiasharaTanzania (TanTradeyanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.

23
Bw. Emmanuel Maishaa Afisa Matekelezo Kanda ya Dar es Salaam akihojiwa na waandishi wa habari wa kituo cha Luninga cha Chanel Ten waliotembelea katika banda hilo.
4
Bw. Juma Milinga Afisa Matekelezo Mwandamizi LAPF akihojiwa na waandishi wa habri wa Chanel Tena ili kuelezea mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo katika maonyesho ya Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
5
Kushoto  ni Simboninsia Ndosi Afisa Mafao Mwandamizi LAPF  akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda hilo kulia ni Sophia Matangalu Ofisa Mafao  LAPF wakiwa katika maonyesho hayo ili kutoa maelezo mbalimbali kwa wateja wanaotembelea kwenye banda hilo.
6
Afisa Matekelezo LAPF Bi. Agness William akitoa maelezo kwa  wateja mbalimbali wanaotembelea katika banda hilo wakati huu wa maonyesho ya sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
7
Bw. John Mwita Afisa Matekelezo Kanda ya Dar es salaam akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda hilo.
8
Afisa Mwandamizi wa Mawasiliano LAPF Bi. Rehema Mkamba akijadiliana jambo na Agness William Afisa Matekelezo.
9
Baadhi ya wateja wakipata maelezo mbalimbali wakati walipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam
10
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa LAPF Bi. Agnes William akihijiwa na Hajra Kondo mwandishi wa kituo cha Televisheni cha TV 1 wakati waandishi hao walipotembelea katika banda hilo.

No comments