Header Ads

Responsive Ads Here

WATANZANIA WATAKIWA KUMUOMBEA MH. RAIS MAGUFULI


Na Mahmoud Ahmad Arusha
Watanzania wametakiwa kujenga busara na uelewa katika kuhakikisha wanakataa kushawishiwa na Shetani ili kudhoofisha juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt John Magufuli  katika vita ya ufisadi na uhujumu wa uchumi anayoendelea nayo hivi sasa.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya la Arusha Gabriel Daqqaro kwenye Kongamano la kumuombea rais lililoandaliwa na kanisa la International evengalism lenye makao makuu Sakila wilayani Meru na kufanyika kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini hapa na kuwasihi viongozi wa dini kuwaeleza ukweli waumini wao juu ya  juhudi za mh rais katika mapambano ya uhuru wa kiuchumi.
Daqqaro amesema kuwa juhudi alizozionyesha mh.rais zinafaa kuungwa mkono na jamii yenye hofu na muumba wetu kwani ndani yake kuna mtihani mgumu unaohitaji kumuweka kwenye maombi yetu ya kila siku sehemu yeyote iwe kazi na hata majumbani kwani wanaopinga wanatembea na shetani.
“hakuna atakayependa haya anayofanya mh.rais akawa upande wa mungu bali atakuwa upande wa shetani hivyo tukiomuona tumkemee kwa nguvu zote kwani wakati wa sasa ni wakati wa mabadiliko ya uchumi” alisema Daqqaro
Nae Askofu wa kanisa la Kiinjili la kilutheri dkta Simon Masangwa alisema kuwa nchi yetu inapita katika kipindi kigumu cha mabadiliko ya kiuchumi yanayohitaji mtu mwenye hofu ya kimungu kama anavyofanya mh. Rais wetu hivyo kama waumini tuwanawajibu mkubwa wa kuwa pamoja na wakati wote kwa kumuombea dua na sala kila siku ili aweze kufanikiwa.
Alisema kuwa suala la kupigania uhuru wa kiuchumi si suala dogo hata kidogo na linahitaji kuungwa mkono na wananchi wote bila kujali itikadi zetu ilikila mmoja aweze kufaidi keki ya nchi yetu.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa la International Evangalism dkta Eliud Isangya alisema kuwa mh. Rais dkta Magufuli ameonyesha uzalendo kwa kutangaza vita vya uhuru wa kiuchumi na ataandikwa katia vitabu vya kumbukumbu ya kihistoria kwa kuukataa utumwa wa kiuchumi hivyo nasi tumeonelea tumuunge mkono kwa kuandaa kongamano hili la kumuombea mungu katika utumishi wake.
Alisema kuwa si wote wanaopenda kuona vita hii inafanikiwa ila kwa umoja wetu na kutoa ushirikiano kwake atafaikiwa katika vita hiyo na tuende mbali katika kulinda amani yetu na umoja wetu  kama watanzania wenye hofu ya mungu.

No comments