Header Ads

Responsive Ads Here

WAONGOZA UTALII WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUWAPENDEKEZA WATAKOINGIA KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUMPATA MUONGOZAJI BORA WA MWAKA 2017


 
Wa kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock
Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of
Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa  wakiwa katika maonyesho
ya (3)Utalii ya Kilifair  katika uwanja wa Chuo cha Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro.Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.
 Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa
ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang’anyiro cha
kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata
Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya
Mashariki na Kati .
Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo
hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo  inafahamika
kama  TANZANIA TOUR GUIDE AWARDS   ambapo
mwaka jana ilikuwa imegawanyika   katika vipengele vya
kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila
mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa
Utamaduni pamoja na Mpishi bora.
Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo
kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza
watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha
katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni
mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii
vilivyopo.
 Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma
ya  utalii hapa nchini waongoza Watalii  hawajawahi kupewa
kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii
huwa  anatumumia 99% ya muda wao  kukaa na mgeni awapo
nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu  hadi anaondoka
nchini. “Ikumbukwe kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma hii ya
utalii waongozaji hawajawahi kupewa kipaumbele wakati anatumia 99%ya
muda wake na mgeni akiwa hapa nchini ,anahakikisha mgeni yupo
salama,anahakikisha mgeni anapata taarifa zote sahihi hadi anaondoka
nchini,muongozaji huyu anafanya kazi yake kama mwalimu,Daktari pale
mgeni anapopata taizo anampatia huduma ya kwanza,mpishi,mpatanishi na
Balozi mwaminifu”.alisema Sadock.
Kwa
upande wake Katibu wa Waongoza watalii wa kujitegemea Ally
Mtemvu amesema kuwa hakuna mgeni anayekuja nchini kufanya utalii
pasipokuwa na muongozaji amesema tuzo hiyo inawashirikishwa
makampuni yote ya utalii ,wadau wa utalii KIATO,TATO, pamoja
KGA,TTGA,FGST,KTAS,TTG,KILIMERU,TPO,MMPA,NCPG na NMPA
” Hivyo
tunaiomba Wizara ya Utalii na Maliasili watuunge mkono kuhakikisha
kuwa tuzo hii ya Afrika Mashariki na Kati zinakuwa bora zaidi kwakuwa
tumewatangulia na imeasisiwa nchini Tanzania “alisema Ally.
Aidha
Tuzo hii ilizinduliwa rasmi mwaka 2016 mkoani Arusha ambapo mgeni
rasmi alikuwa Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Anjelina Madete,ambapo mwaka huu 2017 itafanyika jijini Dar es salaam
kwenye maonyesho ya SITE october 13-15,2017 ambapo mgeni rasmi
atafahamika hapo baadae.
Mwisho wa mapendekezo ya majina ni tarehe
30/6/2017

No comments