Header Ads

Responsive Ads Here

Wanafunzi DIT Washuhudia TBL Group Ilivyojipanga Kuwa Kioo Cha Utekelezaji Sera ya Tanzania ya Viwanda


unnamed
.Wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology( DIT) wakimsikiliza kwa makini  Afisa Usalama Mwandamizi wa TBL Group   Khery Gunzarethy

1
Mtalaam wa upishi wa bia  wa TBL Group Christian Tarimo akiwapatia maelezo ya kitaalamu ya moja ya mchakato wa uzalishaji
2
Mtalaam wa upishi wa bia  wa TBL Group Christian Tarimo akiwaonyesha moja ya mitambo ya  uzalishaji wa bia
 
3
.Wanafunzi  wakisikiliza kwa makini maelezo ya kitaalamu
4
Wanafunzi wakimsikiliza mtaalamu wa maabara Lyidia Soi
5
wanafunzi wa DIT katika picha ya pamoja baada ya kufanya ziara ya mafunzo TBL.
 
……………………….
 
Wanafunzi kutoka Chuo Cha Teknolojia Cha Dar Es Salaam (DIT) wamefanya ziara ya mafunzo katika kiwanda cha TBL cha Ilala na kujionea jinsi TBL Group ilivyojipanga kuwa kioo cha utekelezaji wa sera ya kujenga Tanzania ya Viwanda.
Akiongea na ujumbe wa wanafunzi hao,Afisa  Afisa Usalama Mwandamizi wa TBL Group   Khery Gunzarethy , alisema kuwa wakati serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga Tanzania ya Viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi  na kuongeza fursa za ajira kwa kasi kuna haja ya kuhakikisha kunakuwepo wataalamu wa kubuni na kuendesha mifumo ya kisasa ya biashara ili biashara zitakazoanzishwa zizidi kukua na kuwa endelevu.
  Gunzarethy  Alisema biashara yoyote inayoendeshwa kwa kufuata misingi ya kitaalamu ni lazima ipate mafanikio na kuwa endelevu “Biashara ikiendeshwa kwa misingi ya kitaalamu inakua kwa haraka na kuchangua kukuza uchumi wa nchi,kuongeza wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,kuchangia pato kubwa kwa serikali kwa njia ya kulipa kodi na kunufaisha jamii kwa namna mbalimbali”.
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa TBL Group kupitia viwanda  vyake vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kiasi kikubwa imekuwa ikizingatia kuendesha shughuli zake kwa kufuata misingi bora ya uendeshaji biashara ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kampuni kupata mafanikio mengi na kuwa kioo cha uwekezaji bora ambapo watu kutoka sehemu kadhaa wamekuwa wakitembelea viwanda vyake kwa ajili ya kujifunza mifumo ya uzalishaji bora wenye tija na ufanisi.
 
 “Kampuni ya TBL Group imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa kodi,utunzaji wa mazingira,kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia mtandao wa biashara zake,kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo inaoshirikiana nao,kuendesha kampeni ya unywaji wa kistaarabu kwenye jamii,kuwezesha wakulima ambao wanaiuzia malighafi na imekuwa kinara wa kutekeleza kanuni bora za ajira ambapo imekuwa ikishikia rekodi ya kupata tuzo ya Mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri nchini (ATE)”.Alisema.
 
 
 
Aliongeza kuwa mafanikio haya hayatokani na kufuata mifumo bora ya uzalishaji pekee bali ni kuwa na wafanyakazi wenye vipaji vikubwa na taaluma mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa kujituma wakati huohuo kampuni ikiwa inawapatia motisha na mafunzo ya  kwa mara ili kuhakikisha wakati wote wanakwenda na wakati  sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku.
 
 Aliwaeleza kuwa TBL Group chini ya kampuni mama ya AbInBev itaendelea kufanya kazi sambamba na serikali,taasisi zingine na  wananchi kwa ujumla kwenye jamii kuhakikisha  maendeleo endelevu yanapatikana na aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili wapate elimu nzuri itakayowawezesha kushindana katika soko la ajira ikiwemo kujiajiri kupitia taaluma zao

No comments