Header Ads

Responsive Ads Here

WAKAZI WA JIMBO LA MJI WA KIBAHA WAMPA SALUTE KOKA


KOKA1
Picha mbalimbali zikionyesha vifaa tiba mbalimbali vilivyogharimu mil.400 ,vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,ambapo vitagawiwa katika zahanati na vituo vya afya 11 vilivyopo mjini hapo ikiwemo Kituo cha afya Mkoani .(picha na Mwamvua Mwinyi)

KOKA2KOKA3
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WAKAZI wa jimbo la Kibaha,mkoani Pwani wamesema kitendo cha mbunge wao Silvestry Koka kutoa msaada wa kontena la vifaa tiba vyenye thamani ya sh.milioni 400 itasaidia kuondoa upungufu wa vifaa tiba .
Wamesema viongozi wa kuchaguliwa wanatakiwa kutimiza ahadi zao walizoziahidi wakati wanaomba kura .
Msafiri Mgeni ameeleza ,akina mama wajawazito ,watoto hasa walikuwa wakipata adha ya uhaba wa vifaa tiba kwenye wodi ya uzazi lakini kwa sasa itakuwa imepunguza makali .
Nae mbunge wa jimbo la mji wa Kibaha ,Koka alisema vifaa hivyo vipo 831 na vitagawiwa katika kituo cha afya cha Mkoani na zahanati 11 zilizopo halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Akimkabidhi vifaa hivyo, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo ili kukabiliana na upungufu wa vifaa tiba.
Koka alifanikiwa kupata vifaa hivyo kupatia shirika na la Project Cure na marafiki zake walioko nchini Marekani ambao wanafadhili vifaa tiba kwa nchi zinazoendelea.
Alieleza kuna vifaa takriban 831 vya aina tofauti ambavyo vilikuja kwenye kontena la futi 40 vitasambazwa kwenye kituo hicho pamoja na zahanati .
“Wao walitaka tutoe gharama za usafirishaji kutoka Marekani hadi Tanzania ambapo mimi nimetoa milioni 12 na Halmashauri ilitoa milioni 32 huku vifaa hivyo vikiwa na gharama ya shilingi milioni 400,” alisema Koka.
“Nimeamua kuwatumikia wananchi wangu kwa kufanikisha vifaa hivyo na hatimaye vimepatikana na kama mnavyoona viko ,” alisisitiza .
Alisema kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo kutasaidia mchakato wa kukifanya kituo hicho cha Afya kuwa Hospitali ya wilaya kwani bila ya kuwa na vifaa haiwezi kupanda hadhi .
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla alielezea ,vifaa hivyo ni vya kisasa na watumishi wa Idara ya afya wanapaswa kuvitumia vizuri ili viwe na manufaa na kuondoa changamoto zilizopo.
Alisema vifaa hivyo vinapaswa kutunzwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwenye ripoti ambayo itapelekwa wizarani kwa ajili ya kumbukumbu ili visije vikaibiwa na wajanja.
Dk.Kigwangalla aliwataka wabunge wengine kuiga mfano wa Koka ambae amekuwa mbunifu kuwatumikia wananchi wake .
Aliwaasa watu wanaojitokeza kuonyesha nia ya kugombea ubunge jimboni hapo kwasasa  na kudai ni wakati wa kumuacha Koka afanye kazi na kutekeleza ilani ya CCM kama alivyoanza .
Pia dk.Kigwangalla aliwaomba wananchi na wanaCCM kuacha kubadilisha viongozi wa kuchaguliwa kama wabunge ambao wanafanya kazi waache katika kipindi fulani ili watimize malengo yao .
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Kibaha Diwani wa Kata ya Sofu Yusuf Mbonde alisema kupatikana kwa vifaa hivyo Koka kafanya jambo la kishujaa kwani atawaondolea adha wananchi .

No comments