Header Ads

Responsive Ads Here

UJUE WASIFU BABKUBWA WA PROFESA MWANDOSYA PROFESA MARK MWANDOSYA

 Kwa hakika kabisa. Cv hii imeshiba. Nimefurahishwa na WASIFU na MAELEZO BINAFSI YA PROFESA M. J. MWANDOSYA, 

Naamua kumpatia heshima kubwa ya uwezo alionao kielimu na Mungu ambariki sana. A: Binafsi Jina: MWANDOSYA, Mark James Tarehe ya Kuzaliwa: 28 Desemba, 1949 Mahali pa kuzaliwa: Mbeya Maelezo ya Familia: Nimeoa na tuna watoto watatu na wajukuu wawili. B: Elimu Elimu ya Msingi: Shule ya Msingi Majengo, Mbeya, 1957 – 1958 Shule ya Msingi Chunya, 1959 – 1960 Shule ya Kati Chunya, 1961 – 1964 Elimu ya Sekondari: Shule ya Sekondari Malangali, 1965 – 1968 Chuo vcha Ufundi Dar es Salaam, 1969 - 1970 Elimu ya Juu: Chuo Kikuu cha Aston, Uingereza, 1971-1974 Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, 1974-1977 Shahada: Shahada ya Uhandisi Umeme ya Chuo Kikuu cha Aston (Bachelor of Science 1st Class Honours, University of Aston), 1974 Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu cha Birmingham (Doctor of Philosophy in Electronic and Electrical Engineering, University of Birmingham), 1977 C: Uzoefu katika kazi na Uongozi i. Kazi: 1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) 2012 2. Mkuu (Chancellor), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology-MUST) (2014-mpaka sasa) 3. Waziri wa Maji (2010-2012) 4. Waziri wa Maji na Umwagiliaji (2008-2010) 5. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) (2006-2008) 6. Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi (2000-2005) 7. Mbunge wa Rungwe Mashariki (2000 – 2015) 8. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (2002 – mpaka sasa) 9. Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara, (1992-1993) 10. Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini, (1990-1992) 11. Kamishna wa Nishati na Petroli, Wizara ya Nishati na Madini (1985-1990) 12. Mkurugenzi, Kituo cha Nishati, Mazingira, Sayansi na Teknolojia (CEEST), (1993-2000) 13. Profesa wa Uhandisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1987-2000) 14. Profesa Mshiriki wa Uhandisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1983-1987) 15. Mtafiti (Sayansi), Chuo Kikuu cha Princeton, Marekeni, (1983-1984) 16. Mhadhiri Mwandamizi (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1980- 1983) 17. Mhadhiri (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1977-1980) 18. Mhandisi, Kampuni ya General Electric Company, Manchester, Uingereza, (1977- 1978) 19. Mhadhiri Msaidizi (Uhandisi Umeme), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1976- 1977) ii. Uongozi: 1. Mjumbe, Bodi ya Usimamizi wa Jopo la UNEP la Kimataifa la Matumizi Bora ya Rasilimali (UNEP International Resource Panel). 2. Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Nyakati tofauti,( 2000-2005) 3. Mwenyekiti, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (1996-2000) 4. Mwenyekiti, Kituo cha Nishati, Mazingira, Sayansi na Teknolojia, (1993-2000) 5. Mwenyekiti, Kampuni ya Siemens (Tanzania) Ltd, (1999-2000) 6. Mwenyekiti, Kampuni ya Kibo Paper Industries Ltd, (1995-1998) 7. Mwenyekiti, Kampuni ya Williamson Diamond Company Ltd, (1990-1992) 8. Mwenyekiti, Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, (Tanzania Industrial Research and Development Organisation), (1994-1998) 9. Mwenyekiti, Tanzanian and Italian Petroleum Refinery (TIPER), (1987-1993) 10. Mwenyekiti, Mamlaka ya Maji Mijini (NUWA), (1991-1993) 11. Mwenyekiti, Bodi ya Utawala ya Chuo cha Biashara, (1992-1993) 12. Mwenyekiti, Kampuni ya Gesi (GASCO), (1998 -2000) 13. Mwenyekiti, Kamati ya kutayarisha Sera ya Nishati, (1988-1991) 14. Mwenyekiti wa Kundi la nchi zinazoendelea (G77) na Msemaji Mkuu wa nchi hizo na China katika majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yailyo fanikisha kupatikana kwa Itifaki ya Kyoto,(1997) 15. Mwenyekiti, Timu iliyoandaa Itifaki ya Sekta ya Nishati ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) 16. Makamu Mwenyekiti, Tume ya Taifa ya UNESCO, (1983-1988) 17. Makamu Mwenyekiti, Shirika la Maendeleo ya Taifa, (National Development Corporation-NDC), (1992-1993) 18. Makamu Mwenyekiti, Bodi ya Wadhamini, Southern African Development through Electricity (SADELEC) ya Afrika ya Kusini, (1994-1998) 19. Kamishna, Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirkia ya Umma, (1996-1999) 20. Kamishna, Tume ya Mawasiliano, (1999-2000) 21. Mkurugenzi, TAZAMA Pipeline Lted, (1987-1993) 22. Mkurugenzi, National Textile Corporation TEXCO, (1993) 23. Mkurugenzi, Tanzania Zambia Railway Authority TAZARA, (1992-1993) 24. Mkurugenzi, Shirika la Posta na Simu, TPTC, (1981-1986) 25. Mkurugenzi, Shirika la Ugavi wa Umeme, Tanesco, (1985-1990) 26. Mkurugenzi, Shirika la Maendeleo ya Petroli, TPDC, (1985-1990) 27. Mkurugenzi, Kilwa Ammonia Company Ltd (KILAMCO), (1985-1990) 28. Mkurugenzi, Standard Chartered Bank Tanzania Ltd, (1999-2000) 29. Mkurugenzi, AGIP (Tanzania) Ltd, (1989-1991) 30. Mjumbe, Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (1994-2000) 31. Mjumbe, Baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (1994-2000) 32. Mjumbe, Baraza la Utawala IDM-Mzumbe, (1992-1993) 33. Mjumbe, Baraza la Utafiti wa Kisayansi (Tanzania National Scientific Research Council), (1981-1983) 34. Mjumbe, Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia, (Tanzania Commission for Science and Technology), (1987-1990) 35. Mjumbe, Timu ya kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. 36. Mjumbe, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, (National Environment Management Councli-NEMC), (1999-2000) iii. Uwakilishi wa Nchi katika Mikutano ya Kimataifa 1. Mkutano Mkuu wa 20 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Paris, France, Novemba, 1978 2. Mkutano Mkuu wa 21 wa UNESCO, Belgrade, Yugoslavia, Oktoba 1980 3. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nishati mpya ya Nishati Mbadala, Nairobi, Kenya Agosti, 1981. 4. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nishati Mbadala, Rome, Italia, June 1982 5. Mkutano Mkuu (wa 4 wa dharura) wa UNESCO, Paris, Novemba, 1981 6. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nishati Mbadala, New York, Mei, 1984 7. Mkutano wa UNESCO wa Mawaziri wa Afrika wa Sayansi na Teknolojia, Arusha, Julai, 1987 8. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Berlin, Ujerumani, Aprili, 1995 9. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Geneva, Uswisi, Desemba, 1996 10. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Kyoto, Japan, Novemba, 1997. 11. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa Buenos Aires, Argentina, Oktoba, 1998 12. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, Bonn, Ujerumani, Oktoba, 1999 13. Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa, Bali, Indonesia 2009 14. Mikutano ya Maafisa na ya Mawaziri wa Nishati na Madini katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, (SADC), 1985-1992 15. Mikutano ya Maafisa na ya Mawaziri wa Biashara na Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, 1993 16. Mikutano ya Maafsia na ya Mawaziri wa Biashara na Viwanda ya Preferential Trade Area (sasa COMESA), 1993. 17. Nimeongoza ujumbe wa Tanzania katika majadiliano na Benki ya Dunia (World Bank) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank (AfDB) kuhusu mikopo nafuu kuendeleza na kuboresha usambazaji wa umeme na petroli, 1988-1992 18. Nimeongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya Kimataifa inayohusu usafiri wa anga, maendeleo ya simu duniani, bandari, maendeleo ya reli, mazingira, maji na umwagiliaji. 19. Nimehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa kuhusu Habari na Mawasiliano, Geneva, Uswisi, Desemba 2003 nikimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 20. Mkutano Mkuu wa Shirika la Biashara (WTO), Hong Kong, 2005. D: Ushauri (Consultancy) i. Nimetoa ushauri wa kitaalam kwa vipindi mbalimbali kwa Serikali za nchi zifuatazo: Nambia, Zimbabwe, Eritrea ii. Nimetoa ushauri wa kitaalam kwa mashirika ya Kimataifa yafuatayo: UNDP, UNEP, UNESCO, GTZ, USCSP, GEF, SADC, OAU, UNECA iii. Niliongoza timu ya wataalam tulioandaa Itifaki ya Ushirkiano katika Nishati katika nchi za SADC iv. Niliandaa rasimu ya kwanza ya Mkataba wa ushirikiano katika Nishati na Maliasili wa Umoja wa Nchi za Kiafrika (OAU) E: Uzoefu katika Siasa 1. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (2002 – mpaka sasa) 2. Mwanachama wa CCM (1977 mpaka sasa) 3. Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Umoja wa Vijana wa CCM Ofisi Ndogo ya Makao Mkuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, (2000 -2005) 4. Naibu Kamanda, Vijana wa CCM Wilaya ya Rungwe (1998 mpaka Machi 2000) 5. Mwanachama wa TANU (1971-1977) 6. Mwanachama, Umoja wa Vijana wa TANU (1967-1971) 7. Mwanachama, Umoja wa Vijana wa TANU (1967-1971) 8. Makamu wa Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa TANU, Tawi la Shule ya Sekondari ya Malangali, (1967-1968) 9. Mwenyekiti Umoja wa Wanafunzi wa Afrika, Chuo Kikuu cha Birmingham, 1975 F: Mada, Maandishi, na Vitabu 1. Mada: Nimeandika na kuchapisha mada 36 katika majarida ya kitaalamu nchini na nchi za nje. 2. Ripoti za Utaifiti: Ripoti 12 za utafiti mbalimbali zimechapishwa ndani na nje ya nchi. 3. Uhariri: nimehariri majarida na vitabu 9 4. Vitabu: nimeandika vitabu 10 katika uhandisi, nishati, mazingira na maendeleo.

No comments