Header Ads

Responsive Ads Here

TIOTE AANGUKA GHAFLA NA KUFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE MAZOEZI NI KIUNGO WA IVORY COAST


41210C3900000578-0-image-m-125_1496678363265
Kiungo wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote ameanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa mazoezini.
Tiote amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa mazoezini katika kikosi cha Beijing Enterprises kinachoshiriki ligi daraja la pili.
Kiungo huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na timu hiyo miezi mine tu iliyopita.
Alikimbizwa hospital zikiwa ni juhudi za kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana.
Tiote amewahi kuwa kiungo tegemeo wa timu ya taifa ya Ivory Coast iliyokuwa inaongozwa na Didier Drogba.

No comments