Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 11.06.2017 majira ya saa 13:30 Mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko katika Kijiji cha Muungano kilichopo Kata ya Ikolo, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la ZELA GODFREY [40] Mkazi wa Mbugani Wilaya ya Kyela akiwa na Pombe Moshi ujazo wa lita 11 na nusu.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na Pombe hiyo akiwa kwenye harakati za kuisafirisha akiwa amehifadhi kwenye vidumu na ma box ya sabuni. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI]
Mnamo tarehe 11.06.2017 majira saa 01:00 usiku huko katika eneo la Chimala Check Point, Kata ya  Chimala,  Tarafa ya Ilongo,  Wilaya ya Mbarali,   Mkoa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni   1. BENEDICT DANNY @ KYANDO [24] Mkazi wa Matamba – Uwanji, Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe na mwenzake 2. HIRAD NOAH @ SIGARA [22] Dereva Bodaboda na Mkazi  wa Matamba,  Makete – Njombe, wakiwa na bhangi debe mbili iliyohifadhiwa ndani ya box.
Watuhumiwa wamekamatwa wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani. 
WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kuacha kutumia Pombe haramu ya Moshi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili watuhumiwa wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
                                             Imesainiwa na:
 [DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments