Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 29.06.2017. 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 28.06.2017 majira ya saa 13:30 Mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako katika maeneo ya Mtaa wa Ibara na Iwambala iliyopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga Jijini Mbeya.
Katika misako hiyo watuhumiwa wawili ambao ni 1. NDUMIGWA MWAMBUGUSI [65] Mkazi wa Ibara na 2. FRANK NJEBELE [38] Mkazi wa Iwambala wakiwa na Pombe Moshi [Gongo] ujazo wa lita 28 na nusu.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA DAWA ZIDHANIWAZO ZA KULEVYA.
Mnamo tarehe 28.06.2017 majira saa 19:30 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako maeneo ya CCM Tukuyu na Igogwe iliyopo Kata ya Bulyaga na Kawetere, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Katika misako hiyo, watuhumiwa watatu walikamatwa ambao ni 1. FELIX OSWARD [42] Mkazi wa Msasani – Tukuyu akiwa na kete 8 za unga udhaniwao dawa za kulevya 2. NURU WILIAMU [23] na SIMON NGAILO [19] wote wakazi wa Igogwe wakiwa na unga udhaniwao kuwa dawa za kulevya kete 17 pamoja na sarafu Tshs. 258,150/=.
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Kumekuwa na tukio 01 la mauaji kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 27.06.2017 majira ya saa 19:30 usiku huko  Kitongoji cha Maonde, Kijiji cha Sipa, Kata Kambikatoto, Tarafa Kipembawe, Wilaya ya  Chunya, Mkoa wa Mbeya.  Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la NYANGABO RAMADHANI [36] Mkazi wa Maonde aliuawa kwa kukatwa panga kichwani akiwa nyumbani kwake mtu/watu wasiofahamika.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu alikuwa akimtuhumu mtuhumiwa aitwaye LIFA JISANDU [44] Mkazi wa Maonde kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo aitwaye ASHA OMARY [28] Mkazi wa Maonde. Mtiliwa shaka mtuhumiwa mmoja LIFA JISANDU, amekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya. Upelelezi unaendelea.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kuacha kutumia Pombe haramu ya Moshi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili watuhumiwa wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
                                                Imesainiwa na:
 [DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments