Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


  • WATOTO WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA KUJERUHI MMOJA KATIKA AJALI YA MOTO ULIOUNGUZA NYUMBA WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 21.06.2017 MAJIRA YA SAA 22:30HRS KATIKA MTAA WA KIGOTO KATA YA KIRUMBA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATOTO WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.DAUD SAID MIAKA 07, MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI  YA SONGA MBELE NA 2.SOPHIA SAID MIAKA 05, WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ULIOZUKA GHAFLA WAKATI WAKIWA WAMELALA NA KUWAUNGUZA HADI KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO KISHA KUJERUHIWA MAMA WA WATOTO HAO AITWAYE NAOMI PAUL  KWENYE  MAENEO YA MIKONO NA USONI WAKATI AKIJARIBU KUWAOKOA WATOTO WAKE NA KUFANYA UHARIBIFU WA MALI NA VITU AMBAVYO THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.

INADAIWA KUWA BAADA YA KUPATA CHAKULA CHA USIKU MAMA MWENYE WATOTO BI NAOMI PAUL ALIWAPELEKA WANAE WA NNE CHUMBANI KULALA, HUKU YEYE AKIENDELEA NA SHUGHULI NDOGO NDDOGO NJE YA NYUMBA YAKE.  AIDHA INASEMEKANA KUWA WAKATI AKIWA NJE ALISHANGAA KUONA MOTO MKUBWA NDANI YA NYUMBA YAKE CHUMBANI WALIPO LALA WANAWE, NDIPO BAADA YA KUONA HALI HIYO ALIINGIA  NDANI KWENDE KUWAOKOA WATOTO WAKE HUKU AKIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA, LAKINI  MOTO ULIKUWA  MKUBWA AMBAPO ALIWEZA KUWAOKOA WATOTO WAWILI TUU, HUKU WENGINE WAWILI TAJWA HAPO JUU WAKITEKETEKEA KWA MOTO.
WANANCHI WALIFIKA ENEO LA TUKIO  KUTOA MSAADA  KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI  PAMOJA NA JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI, LAKINI MOTO ULIKUWA MKUBWA  HALI ILIYOPELEKEA KUSHINDWA KUUMUDU NA KUTEKETEKEZA NYUMBA YOTE, KWANI MIUNDO MBINU YA ENEO LA NYUMBA ILIPO HAIKUWA RAFIKI.
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWA CHANZO CHA AJALI HIYO YA MOTO NI HITILAFU YA UMEME, AIDHA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKINA NA JESHI LA ZIMA MOTO NA TANESCO WANAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA MSIBA WALIOUPATA. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUWA WAVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMBAPO VYOMBO VYA DOLLA VINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUWA NA UTARATIBU WA KUKAGUA MIUNDOMBINU YA UMEME KATI NYUMBA ZAO ILI KUEPUSHA AJALI ZA AINA KAMA HII.


IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments