Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


  • MTOTO MMOJA MDOGO AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO WILAYANI MISUNGWI

  • WATU WA NNE RAIA WA BURUNDI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUISHI NCHINI BILA KIBALI WILAYANI SENGEREMA.
KWAMBA TAREHE 18.06.2017 MAJIRA YA SAA 19:00HRS KATIKA KIJIJI CHA MBELA KATA NA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, MTOTO MDOGO WA KIUME ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FARAJA SIMON, UMRIA WA MWEZI MMOJA, AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ULIOUUNGUZA CHUMBA ALICHOKUWA AMELAZWA HAPO NYUMBANI KWAO PAMOJA NA KUUNGUZA VITU MBALIMBALI.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI KWA MAMA MLEZI BI EVA MNARI MIAKA 37, MKAZI WA KIJI CHA MBELA KWANI MWEZI ULIOPITA MAMA YAKE MZAZI ALIFARIKI DUNIA. INASEMEKANA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MAMA MLEZI ALIMLISHA CHAKULA KISHA ALIMPEKA CHUMBANI KULALA HUKU YEYE AKITOKA NJE KUENDELEA NA SHUGHULI NYINGINE,WAKATI MAMA MLEZI AKIWA NJE ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ALIONA MOTO NA MOSHI MWINGI UKITOKEA CHUMBANI ALIPOLALA MAREHEMU NDIPO ALIITA WATU WAJE KUMSAIDIA KUUZIMA MOTO HUO.
WANANCHI WALIFIKA NA KUFANYA UOKOAJI KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA UOKOAJI, LAKINI TAYARI MOTO ULIKUA UMEUNGUZA GODORO LILILOKUWA AMELAZWA  MAREHEMU NA KUMUUNGUZA HALI ILIYOPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAKIJA FAHAMIKA, POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA FAMILIA KWA MSIBA WALIOUPATA, ANAOMBA WAWE WAVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI AMBAPO VYOMBO VYA DOLA VINAENDELEA NA UCHUNGUZI ILI KUWEZA KUFAHAMU CHANZO CHA MOTO HUO.
KATIKA TUKIO LA PILI.
MNAMO TAREHE 19.06.2017 MAJIRA YA SAA 08:00HRS KATIKA KISIWA CHA KISABA KATA YA MAISOME WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WA NNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.CHIMIBINANA KORADI, MIAKA 15, MRUNDI, 2.NIYONZIMA CHARLES, MIAKA 18, MRUNDI, 3.NIYONZIMA AUGUSTINO, MIAKA 17, MRUNDI NA 4.NDABAZANIE INOCENT, MIAKA 31, WOTE RAIA WA NCHI YA BURUNDI, AMBAO WANAISHI NCHINI BILA KIBALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO YA KISIWA TAJWA  HAPO JUU WAPO WATU WANAOISHI KISIWANI HAPO NA KUFANYA SHUGHULI MBALIMBALI LAKINI SIO  RAIA WA TANZANIA. AIDHA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIZO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI MAENEO YA KISIWA HICHO NA KUANZA KUFANYA UPELELEZI AMBAPO BAADAE WALIWEZA KUBAINI NYUMBA WALIPOKUWA WAKIISHI RAIA HAO WA NCHI YA BURUNDI NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHIMIWA WOTE WA NNE, AIDHA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA KATIKA IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAFUATA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWAPONGEZA WANANCHI KWA USHIRIKIANO MZURI WANAOUTOA KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU WA AINA KAMA HII AMBAZO ZIMESAIDIA POLISI KUKAMATA WAHALIFU HAO, HIVYO ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LAO ILI LIWEZE KUENDELEA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA WETU.


IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments