Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA


  • MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTOTO WAKE WILAYANI SENGEREMA.

  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI (GONGO) KIASI CHA LITA 23 WILAYANI NYAMAGANA.
MNAMO TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU KATIKA KISIWA CHA NYAMANGO KIJIJI CHA SOSWA TARAFA YA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, NYAMISI BAHATI, MWANAMKE, MIAKA 27, MKAZI WA KISIWA CHA NYAMANGO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTOTO WAKE AITWAYE SAKIMU HASSANI JINSIA YA KIUME MWENYE UMRI WA MIEZI SABA, HII NI BAADA YA KUMTUPA MAJINI KWENYE ZIWA VICTORIA NA KUPELEKEA MTOTO KUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA AMBAYE NI MAMA WA MTOTO ALITOKA NYUMBANI KWA MUMEWE NA KWENDA KUWASALIMIA WAZAZI WAKE HUKU AKIWA NA MTOTO WAKE. INADAIWA KUWA AKIWA HAPO NYUMBANI KWAO USIKU MAJIRA TAJWA HAPO JUU ALITOKA NJE AKIWA NA MTOTO KAMA ANAKWENDA KUMBEMBELEZA NDIPO BAADA YA MUDA KUPITA ALIRUDI NDANI AKIWA HANA MTOTO, KUTOKANA NA HALI HIYO BIBI WA MTOTO YAANI MAMA MZAZI WA MTUHUMIWA ALIMUULIZA MTOTO AMEMUWEKA WAPI NDIPO MTUHUMUWA ALIONEKANA AKIWA NA MASHAKA HUKU AKISHINDWA KUONESHA MAHALI ALIPO MTOTO NDIPO BAADAE ALISEMA AMEMTUPA KWENYE ZIWA VICTORIA.
INASEMEKANA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUSEMA HIVYO, BIBI WA MTOTO ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA KWA WATU WEWEZE KUJA KUMUOKOA MTOTO, WANANCHI WALIFIKA MAHALI HAPO KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI. POLISI WALIFIKA KWA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO AMBAPO WALISHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANYA KAZI YA KUMTAFUTA MAJINI NA BAADAE WALIFANIKIWA KUMPATA KISHA WALIMTOA  MAJINI KWENYE ZIWANI VICTORIA LAKINI AKIWA TAYARI AMEPOTEZA MAISHA.
AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO ANASUMBULIWA NA MATATIZO YA AKILI, POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWAOMBA KUWA WAANGALIFU  NA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI WAKATI WOTE ILI WASIJE KULETA MATATIZO YA AINA KAMA HII KWA WATU WENGINE. AIDHA PIA ANAENDELEA KUWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU  ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
 KATIKA TUKIO LA PILI;
KWAMBA TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 20:00HRS KATIKA MTAA WA MALULU – IGOGO WILAYA YA  NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMTA  GHATA CHACHA, MIAKA 36, MWANAMKE, MKAZI WA MTAA WA MALULU – IGOGO, AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI (GONGO) KIASI CHA LITA 23, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.
AWALI ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU YUPO MTU AMBAE ANAJIHUSISHA NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA GONGO, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI MAENEO HAYO HUKU WAKIFANYA UPELELEZI NDIPO BAADAE WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KIASI HICHO CHA POMBE YA GONGO.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE AMBAO WANAJIHUSISHA NA UHALIFU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WETU BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUFANYA KAZI ZILIZO HALALI ZA KUWAINGIZIA KIPATO NA SIO VINGINEVYO, KWANI ENDAPO MTU ATABAINIKA ANAJIHUSISHA  NA SHUGHULI ZA AINA KAMA HII HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENGINE.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments