Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


msangii-1
TAREHE 25.06.2017 MAJIRA YA SAA 16:00HRS KATIKA MTAA WA MKUDI KATA YA NYAMANORO WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, LUSATO JAMES MIAKA 29, MKAZI WA MTAA WA MKUDI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA KAKA YAKE JINA TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 07, MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI YA MKUDI NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI KATIKA SEHEMU ZA SIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI PAMOJA NA FAMILIA YA KAKA YAKE KWENYE NYUMBA YAO YA FAMILIA, INASEMEKANA KUWA MTOTO ANAYEDAIWA KUBAKWA ALIKUWA NA TABIA YA KWENDA CHUMBANI KWA BABA YAKE MDOGO KUCHEZA, KUTOKANA NA HALI HIYO INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTOTO ALIONEKANA AKITOKA KWENYE CHUMBA CHA BABA YAKE MDOGO HUKU AKIWA ANALIA NDIPO ALIPOULIZWA ALISEMA BABA YAKE MDOGO AMEMBAKA.
KUTOKANA NA HALI HIYO WAZAZI WA MTOTO WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI ALIYEBAKWA AMEPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI YA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI AU WALEZI AKIWATAKA KUWA MAKINI NA WATOTO WAKATI WOTE NA WATU/NDUGU WANAO WAZUNGUKA KWANI BAADHI YAO WAPO WENYE NIA OVU ZA AINA KAMA HII DHIDI YA WATOTO, LAKINI PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE 25.06.2017 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA MTAA WA NYASHANA KATA YA MBUGANI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, INNOCENT LAMECK @CLEMENT MIAKA 22, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIJANA AITWAYE SANGIJA GEORGE MIAKA 27, KINYOZI WA MTAA WA NYASHANA, YALIYOTOKANA NA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI WAKATI ALIPOKWENDA KUMUOKOA MDOGO WAKE ASIBAKWE NA MTUHUMIWA PINDI ALIPOKWENDA KUJISAIDIA CHOONI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADIWA KUWA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO ALIKUWA AMEPEWA HIFADHI YA MALAZI YA MUDA HAPO NYUMBANI KWAO MAREHEMU KWANI SEHEMU ALIPOKUA AMEFIKIA HAPAKUWA NA NAFASI, INASEMEKANA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MDOGO WA MAREHEMU WA KIKE JINA TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 12, MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO SHULE YA MSINGI NYASHANA ALIKWENDA CHOONI KUJISAIDIA NDIPO MTUHUMIWA ALIMFUATA CHOONI KISHA ALIANZA KUMBAKA.
INASEMEKANA KUWA WAKATI MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO ANATEKELEZA TUKIO LA UBAKAJI HUKO CHOONI BINTI ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA, MAREHEMU ALIPOSIKIA ALIKWENDA CHOONI KUMUOKOA MDOGO WAKE NDIPO ALICHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KINACHODAIWA KUWA NI KISU NA MTUHUMIWA SHINGONI NA KUFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIKIMBIZWA  HOSPITALI.
WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUOA CHA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANA NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUPOKEA WAGENI WASIO WAFAHAMU KWENYE MAKAZI YAO KWANI WAPO BAADHI YAO WENYE TABIA YA UHALIFU, AMBAO UNAUNAWEZA KUSABABISHA MAJERUHI NA VIFO KWA WATU WASIO NA HATIA. AIDHA PIA ANATOA POLE KWA NDUGU NA WANAFAMILIA KWA MSIBA WALIOUPATA ANAWAOMBA WAENDELEA KUWA WAVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMBACHO WANAPITIA KWANI JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO ILI BAADAE MTUHUMIWA AWEZE KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments