Header Ads

Responsive Ads Here

SIMBA YAZIDI KUVUNJA NGOME YA MBAO FC


IMG-20170614-WA0088-640x427
Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kufanya fujo za kuwasainisha mikataba wachezaji kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa VPL pamoja na mashindano ya kimataifa (CAF Confederation Cup).

Simba imemtambulisha golikipa wa Mbao FC Emanuel Elius Mseja baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
Golikipa huyo alikuwa ni namba tatu katika klabu ya Mbao akiwa nyuma ya Musa Ngwegwe ambaye badae alisimamishwa akituhumiwa kwa upangaji matokeo baada ya timu yake kupoteza mchezo dhidi ya Yanga na huku golikipa namba mbili akiwa ni Benedict Haule ambaye amesaini mkataba wa kujiunga na Azam FC.
Kusajiliwa kwa golikipa huyo kunaifanya Simba kuwa na magolikipa watano (Daniel Agyei, Peter Manyika, Denis Richard, Emanuel Elius Mseja pamoja na Aishi Manula ambaye ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
Kwa maana hiyo, lazima baadhi ya wachezaji wa nafasi hiyo waonde kwenye ili kupisha ujio wa Aishi Manula na  Emanuel Elius Mseja.

No comments